Udhalili
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
1 Wakorintho 15:9,10 Maana mimi ni mdogo katika mitume, nisiyestahili kuitwa mtume, kwa sababu naliliudhi Kanisa la Mungu. Lakini kwa neema ya Mungu nimekuwa hivi nilivyo; na neema yake iliyo kwangu ilikuwa si bure, bali nalizidi sana kufanya kazi kupita wao wote; wala si mimi, bali ni neema ya Mungu pamoja nami.
Nakumbuka ule wakati nilipokuwa Mkristo nikiwa na umri wa miaka 36, baada ya kuishi maisha ya kiburi na ubinafsi ndipo nilipojisikia hali ya kutojiamini kwasababu nilizungukwa na Wakristo walioonekana kuwa ni watakatifu sana. Sijui kama umeshajisikia hivyo?
Unafahamu inavyoenda, Unachunguza watu wengine na kujilinganisha nao. Ni kweli, wengine ni wakorofi, wengine wamerukwa na akili, lakini wengi wao wanaonekana kuwa wazuri kuliko ulivyo, wenye fadhili na hekima kuliko wewe. Hiyo kuna wakati inavunja moyo.
Isitoshe, anaweza kuja mtu kama mimi akiongea habari za ufufuko wa Yesu na karama ya uzima wa milele kwa wale wanaomwamini. Lakini swali linakuja …
Je! Mimi ninastahili kweli? Labda sistahili!
Mtume Paulo alijibu swali hilo wakati alipokuwa anaongea habari za ufufuko wa Yesu na namna wanavyomwamini watafufuka tena waishi milele na milele. Sikiliza alivyoandika:
1 Wakorintho 15:9,10 Maana mimi ni mdogo katika mitume, nisiyestahili kuitwa mtume, kwa sababu naliliudhi Kanisa la Mungu. Lakini kwa neema ya Mungu nimekuwa hivi nilivyo; na neema yake iliyo kwangu ilikuwa si bure, bali nalizidi sana kufanya kazi kupita wao wote; wala si mimi, bali ni neema ya Mungu pamoja nami.
Paulo alikuwa amewatesa Wakristo! Alikuwa mhalifu kati ya wahalifu, mdogo kuliko wote. Lakini sasa, angalia, baada ya miaka 2000, bado tunasoma yale aliyoyaandika.
mtu anapomwamini Yesu, anatazamia uzima endelevu. Hakuna chochote kile katika vyote ulivyofanya zamani ambacho kitaweza kukunyanganya ukweli huo. Kwahiyo, inabidi tuwe na maono. Muda umewadia wa kuachana na udhalili. Amina?!
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.