... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Usidanganyike

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

1 Wakorintho 15:4-8 ... na ya kuwa alizikwa; na ya kuwa alifufuka siku ya tatu, kama yanenavyo maandiko; na ya kuwa alimtokea Kefa; tena na wale Thenashara; baadaye aliwatokea ndugu zaidi ya mia tano pamoja; katika hao wengi wanaishi hata sasa, ila baadhi yao wamelala; baadaye akamtokea Yakobo; tena na mitume wote; na mwisho wa watu wote, alinitokea mimi, kama ni mtu aliyezaliwa si kwa wakati wake.

Listen to the radio broadcast of

Usidanganyike


Download audio file

Sisi sote tumewahi kuhudhuria mazishi, Labda kuzika mpendwa, rafiki au mwenzetu yoyote yule.  Desturi za mazishi ni sehemu muhimu ya maombelezo; tena zinasaidia watu kuaga vizuri marehemu.

Ndio, ninafahamu kwamba kutanguliza mada ya kifo na mazishi sio habari inayopendeza.  Lakini univumilie kidogo kwa maana habari njema inakuja kwa sababu leo tunataka kuongea swala la ufufuo.  Sasa, kwa kuwa sisi sote tumeshuhudia kifo cha mtu aliyekuwa karibu nasi, tukamuombelezea, ndio maana inatuwia vigumu kuelewa dhana ya ufufuo; inatuwia vigumu hata kuiamini pia.  Tuangalie mfano wa Yesu … 

1 Wakorintho 15:4-8  … na ya kuwa alizikwa; na ya kuwa alifufuka siku ya tatu, kama yanenavyo maandiko; na ya kuwa alimtokea Kefa; tena na wale Thenashara; baadaye aliwatokea ndugu zaidi ya mia tano pamoja; katika hao wengi wanaishi hata sasa, ila baadhi yao wamelala; baadaye akamtokea Yakobo; tena na mitume wote; na mwisho wa watu wote, alinitokea mimi, kama ni mtu aliyezaliwa si kwa wakati wake. 

Labda umeshajua habari ya wanafunzi wa Yesu, jinsi ilivyowawia vigumu sana kukubali kwamba Yesu amefufuka, lakini baadae wao pamoja na wengine, ma-mia ya watu, walikutana na Kristo aliyefufuka. 

Inabidi ukumbuke kwamba Paulo aliandika barua hii kwa Wakorintho wakati kulikuwa bado kuna watu wengi ambao walikuwa hawa amini taarifa zile. Kwahiyo, usidanganyike, ufufuo ni kweli kabisa.  Kristo amefufuka.  Ni habari njema kabisa, kwasababu maana yake ni kwamba tukimwamini, siku moja sisi pia tutafufuka tena.  

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.