... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Usijichoshe Kupita Kiasi

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Waefeso 2:4,5,8 Lakini Mungu, kwa kuwa ni mwingi wa rehema, kwa mapenzi yake makuu aliyotupenda; hata wakati ule tulipokuwa wafu kwa sababu ya makosa yetu; alituhuisha pamoja na Kristo; yaani, tumeokolewa kwa neema ... Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu.

Listen to the radio broadcast of

Usijichoshe Kupita Kiasi


Download audio file

Inaonekana kwamba njia ya kupiga hatua katika maisha ni kuvutia watu, yaani kuwashawishi kwa uzuri wetu na akili zetu.  Ndio maana mara nyingi wanasema mtu “amejivika na kujipamba kwa ajili ya mafanikio”.

Nilipokutana na mke wangu Jacqui kwa mara ya kwanza, kusema ukweli nilitaka kumshawishi; kumvutia ili nipate fadhili machoni pake.  Hii ni kawaida. Lakini sasa, tangu tulipofunga ndoa miaka 25 iliopita, sitafuti tena kumshawishi hivyo, ahahaha … bali nataka kumbariki.  Kuna utofauti mkubwa kati ya kushawishi na kubariki.  Iko hivi hata kwa Mungu. 

Kuna watu wengi sana wanamwamini Yesu na wanaishi wakibeba mzigo kwamba lazima wajichoshe ili wamvutie, waweze kufidia makosa yote waliyoyafanya jana. Lakini haiko hivi hata kidogo. Kwasababu imeandikwa hivi:

Waefeso 2:4,5,8  Lakini Mungu, kwa kuwa ni mwingi wa rehema, kwa mapenzi yake makuu aliyotupenda; hata wakati ule tulipokuwa wafu kwa sababu ya makosa yetu; alituhuisha pamoja na Kristo; yaani, tumeokolewa kwa neema … Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa  njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu. 

Yamkini unahitaji kusikia hayo leo hii:  Acha kujichosha sana kwa kujaribu kumshawishi Mungu ambaye tayari ameshakukirimia neema yake.  Huwezi kupata fadhili kwake kwa kufanya kazi … ni karama yake inayotolewa bure, aliyokupatia ndani ya Yesu. 

Hatutendi matendo mema ili tuokolewe. Tunatenda matenda mema kwa sababu tumeshaokolewa. 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.


We use cookies to improve your browsing experience, analyse site traffic & personalise content, but we do not track you when you leave this site. To find out how we utilise & protect your data, check out our "Privacy Policy".

Privacy Policy