... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Mahali Unapokimbilia Mara Moja

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Zaburi 6:1-3 BWANA, usinikemee kwa hasira yako, wala usinirudi kwa ghadhabu yako. BWANA, unifadhili, maana ninayauka; BWANA, uniponye, mifupa yangu imefadhaika. Na nafsi yangu imefadhaika sana; na Wewe, BWANA, hata lini?

Listen to the radio broadcast of

Mahali Unapokimbilia Mara Moja


Download audio file

Jaribu kufikiri kwamba, uko ndani ya mtumbwi halafu dhoruba inakuja ghafla.  Upepo mkali unavuma, mawingu yanajikusanya, mawimbi yanaanza kuyumbisha mtumbwi wako … Sasa. utafanyaje?

Dhoruba zile huwa zinatokea kwasababu mbalimbali. Tunafikiri, labda ni bahati mbaya … au tumekosea vibaya … au Mungu alikusudia tu kwasababu anazozijua yeye mwenyewe kwamba muda umewadia tupate dhoruba maishani mwetu. Lakini, mtu anapojikuta ndani ya mtumbwi mdogo na bahari imechafuka mno kwasababu ya dhoruba kali,  Sasa swali ni hili, mtu atafanyeje? 

Kawaida mtu angejaribu kusoza kwa nguvu zaidi au kupiga simu ili apate msaasda. Na kweli, ni jambo la busara kuvaa boya na kupiga firimbi na kurusha mwanga wa kujulisha hatari uliyomo. Lakini, vipi kama dhoruba ni kali kiasi kwamba hakuna mtu wa kukuokoa?

Mara nyingi mimi ninapenda kusoma Zaburi za Mfalme Daudi kwasababu yeye alipitia dhoruba nyingi sana za  kuhatarisha maisha yake.  Sikiliza alivyotamka wakati wa dhoruba fulani: 

Zaburi 6:1-3  BWANA, usinikemee kwa hasira yako, wala usinirudi kwa ghadhabu yako.  BWANA, unifadhili, maana ninayauka; BWANA, uniponye, mifupa yangu imefadhaika.  Na nafsi yangu imefadhaika sana; na Wewe, BWANA, hata lini? 

Hapo Daudi alikuwa katika hali mbaya sana.  Haijalishi ilitokana na nini, hata kama alikosea au la, yeye alifikiri kwamba dhoruba ile ilitokana na hasira ya Mungu, yaani kuadhibiwa na Mungu.  Lakini hata hivyo, katikati ya dhoruba ile, mara moja alimfanya Mungu kuwa kimbilio chake. 

Tumkimbilie Mungu mapema, usisubiri mwishoni, kuna wakati vinashindikana. 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.