... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Unamfuata Nani?

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Mathayo 4:1-4 Kisha Yesu alipandishwa na Roho nyikani, ili ajaribiwe na Ibilisi. Akafunga siku arobaini mchana na usiku, mwisho akaona njaa. Mjaribu akamjia akamwambia, Ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu, amuru kwamba mawe haya yawe mikate. Naye akajibu akasema, Imeandikwa, Mtu hataishi kwa mkate tu, ila kwa kila neno litokalo katika kinywa cha Mungu.

Listen to the radio broadcast of

Unamfuata Nani?

Download audio file

Ni lini tuliamua kwamba hisia zetu zikichanganywa na maadili yanayooza ya dunia hii ndivyo tutakavyoweza kusadikisha au kubatilisha ukweli wa Neno la Mungu? Hii imetokeaje?

Mtazamo huo si kweli?, Madhehebu mengi ya kikristo wameikataa sehemu kubwa ya ukweli wa Mungu – hususani msimamo wake juu ya mema na mabaya – kwa sababu njia za Mungu ni kama zinawasumbua tu. Yaani njia zake zinagongana na fikra za kisasa. Njia zake haziwapendezi, ni kama zimepitwa na wakati machoni pao.

Ebu fikiria ingekuwaje kama Yesu angekuwa na mtazamo kama huo akiwa pale jangwani: 

Mathayo 4:1-4  Kisha Yesu alipandishwa na Roho nyikani, ili ajaribiwe na Ibilisi.  Akafunga siku arobaini mchana na usiku, mwisho akaona njaa.  Mjaribu akamjia akamwambia, Ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu, amuru kwamba mawe haya yawe mikate.  Naye akajibu akasema, Imeandikwa, Mtu hataishi kwa mkate tu, ila kwa kila neno litokalo katika kinywa cha Mungu. 

Muda ule, kwa njaa aliyokuwa nayo Yesu, matamanio yake pamoja na hisia zake, kama vingesababisha apuuze yale Maandiko, mwishowe Yesu angepiga magoti mbele ya Shetani. angefuata njia za ulimwengu huu.  Kamwe asingalienda hadi msalabani na kuteswa kisha kufa ili dhambi zako na zangu zisamehewe. 

Kusema ukweli ingekuwa matokeo yanayotisha lakini hata hivyo, matokeo ya kukataa Neno la Mungu kwa sababu ya ubinafsi, bado yanatisha na kuleta uharibifu mkubwa. Watu wa Mungu wengi wameacha kumfuata Yesu. wanafuata ubinafsi wao.  Usiwe mmoja wa watu kama hawa. 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.