... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Usijidanganye

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Warumi 14:9-12 Maana Kristo alikufa akawa hai tena kwa sabau hii, awamiliki waliokufa na walio hai pia. Lakini wewe je! Mbona wamhukumu ndugu yako? Au wewe je! Mbona wamdharau ndugu yako? Kwa maana sisi sote tutasimama mbele ya kiti cha hukumu cha Mungu. Kwa kuwa imeandikwa, Kama niishivyo, anena Bwana, kila goti litapigwa mbele zangu; na kila ulimi utamkiri Mungu. Basi ni hivyo, kila mtu miongoni mwetu atatoa habari zake mwenyewe mbele za Mungu.

Listen to the radio broadcast of

Usijidanganye

Download audio file

Kuna hatari; tena ni kubwa, kwa kadiri tunavyokomaa katika mahusiano yetu na Yesu na kadiri maagizo yake yanatawala mioyo yetu, tunaweza kujiona bora kuliko watu wote wengine.

Ni kweli kinzani ya maisha.  Kristo anatuita tuwe wanyenyekevu; kuchukua msalaba na kumfuata pale pote atakapotuongoza hata ikitugharimuje.  Na ndivyo alivyofanya yeye mwenyewe wakati alitoa uhai wake kwa ajili ya wewe na mimi. 

Kwa hiyo, sasa umetembea na Yesu kwa muda wa kutosha na umeishazoea.  Kabisa, mavazi hayo ya Kristo ambayo umejivika kwayo yanakufaa vizuri sana … kama vile Maandiko yanavyoshuhudia. 

Kumbe, swala hili la Ukristo, mimi nimeliweza vizuri sasa!  Angalia mama yule ameingia kanisani chelewa.  Hakuchana hata nywele zake vizuri.  Jamani!  Kwa nini hawezi kwenda sambamba na programu? 

Kama tunafikiri hivyo, basi muda umewadia kujikagua: 

Warumi 14:9-12  Maana Kristo alikufa akawa hai tena kwa sabau hii, awamiliki waliokufa na walio hai pia.  Lakini wewe je!  Mbona wamhukumu ndugu yako?  Au wewe je!  Mbona wamdharau ndugu yako?  Kwa maana sisi sote tutasimama mbele ya kiti cha hukumu cha Mungu.  Kwa kuwa imeandikwa, Kama niishivyo, anena Bwana, kila goti litapigwa mbele zangu; na kila ulimi utamkiri Mungu.  Basi ni hivyo, kila mtu miongoni mwetu atatoa habari zake mwenyewe mbele za Mungu. 

Je!  Kwa kweli, unataka kumwelezea kiburi chako na ubora wako mbele zake Bwana siku ile?  Kweli kabisa?! 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.

We use cookies to improve your browsing experience, analyse site traffic & personalise content, but we do not track you when you leave this site. To find out how we utilise & protect your data, check out our "Privacy Policy".

Privacy Policy