... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Kufanana na Yesu Zaidi na Zaidi

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Warumi 8:28,29 Nasi twajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao katika kuwapatia mema, yaani, wale walioitwa kwa kusudi lake. Maana wale aliowajua tangu asili, aliwachagua tangu asili wanfananishwe na mfano wa Mwana wake, ili yeye awe mzaliwa wa kwanza miongoni mwa ndugu wengi.

Listen to the radio broadcast of

Kufanana na Yesu Zaidi na Zaidi


Download audio file

Nauliza, Hivi, Mtu afanyeje ili abadilishe ukweli fulani – hata kutoka kwenye Biblia – ili uwe uongo?  Ni rahisi tu!  Ni kuikata nusu-nusu au kuinukuu bila kuangalia mistari inayotangulia au inayofuata au kufanya yote mawili.  Baba wa uongo ameshakuwa fundi kabisa wa kubadilisha ukweli.

Acha nitoe mfano: 

Warumi 8:28  Nasi twajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao katika kuwapatia mema, yaani, wale walioitwa kwa kusudi lake.   

Haleluya, Bwana asifiwe!  Mambo yote yatakuwa sawa kabisa.  Hongereni!  Yaani ni safi kabisa … hadi mtu anasoma mstari unaofuata: 

Warumi 8:29  Maana wale aliowajua tangu asili, aliwachagua tangu asili wanfananishwe na mfano wa Mwana wake, ili yeye awe mzaliwa wa kwanza miongoni mwa ndugu wengi. 

Mungu ameamua nini? Ameamua tufanane na Mwanae; yule aliyetendewa jeuri na kutoa damu yake pale msalabani na hatimaye kufa.  Kwahiyo majaribu tunayoyapata maishani, badala ya kutusaidia kufikia mipango yetu ya starehe na mafanikio, kumbe yamekusudiwa yatufananishe zaidi na zaidi na Yesu. 

Daima msalaba unatangulia halafu huja ufufuo.  Hayo yanaumiza kwa sababu yale mema Mungu anayotaka atupatie wewe na mimi kupitia milima na mabonde ya maisha haya, na makona yale yanayotusumbua sana, kumbe yana makusudi mema ya hali ya juu. 

Kama vile mtu mmoja alivyosema:  Nimeona kwamba kujaribu kufanana na Yesu inaleta matokeo mazuri kuliko mimi kujaribu kujirekebisha. 

Mungu alikuchagua kabla ya uumbaji.  Na atatenda kazi ili akuletee mema kwa ndani na hata kwa ajili ya ufalme wake kupitia kila jaribu unalolipata.  Lengo lake ni kukufananisha na Yesu zaidi na zaidi. 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.