Usijipendeze Mwenyewe
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Warumi 15:1-3 Basi imetupasa sisi tulio na nguvu kuuchukua udahifu wao wasio na nguvu, wala hatiupasi kujipendeza wenyewe. Kila mtu miongoni mwetu na ampendeze jirani yake apate wema, akajengwe. Kwa maana Kristo naye hakujipendeza mwenyewe; bali kama ilivyoandikwa, Malaumu yao waliokulaumu wewe yalinipata mimi.
Zamani hizi za kujipendeza, wakati watu wengi wanatetea haki zao, ni rahisi sisi nasi kuanza kufanana nao. Lakini tusidhani kwamba hili ni jambo jipya la kushangaza, hapana.
Zamani kwenye karne ya kwanza baada ya Kristo wakati Ukristo ulianza kutoka kwenye dini la Wayahudi, kulikuwa mvutano mkubwa kati ya Wakristo hawa wapya, kuhusu vyakula vilivyo halali, nyama gani zilizo halali na zilizo najisi. Kukawa swali lingine kujua kama mtu anaweza kunywa divai n.k. …
Siku hizi, maswala hayo kwa Wakristo wengi, yameshapatiwa majibu. Lakini wakati tunaanza kuchunguza Andiko hili, tujue kwamba kuna kitu alichotaka kulenga Mtume Paulo, ni kwamba kulikuwa watu baadhi walitaka kutumia uhuru wao mpya walioufurahia bila kuelewa kwamba kwa kufanya hivyo walikuwa wanabomoa imani ya watu wengine.
Warumi 15:1-3 Basi imetupasa sisi tulio na nguvu kuuchukua udahifu wao wasio na nguvu, wala haitupasi kujipendeza wenyewe. Kila mtu miongoni mwetu na ampendeze jirani yake apate wema, akajengwe. Kwa maana Kristo naye hakujipendeza mwenyewe; bali kama ilivyoandikwa, Malaumu yao waliokulaumu wewe yalinipata mimi.
Je! Alitaka kusema nini? Hata kama wewe unafikiri kwamba una haki zote kwa kutenda jambo fulani – yaani una uhakika kabisa kwamba uko sahihi – kwamba kuwa sahihi na kushinda katika mvutano, siyo shabaha ambayo tungelenga. Bali, ni kutafakari kwanza jinsi kutumia haki zako unazoziamini wewe kungeweza kumwumiza jirani yako … hata kama jirani yako hayuko sahihi.
Kwa maneno mengine, ujumbe wa Mungu kwetu ni huu: Usitetee haki zako kama zinaweza kumwumiza mtu mwingine, kama vile Kristo hakujipendeza bali alikubali kwenda msalabani kwa kulipa deni la dhambi zako na la dhambi zangu.
Usiwaumize watu wengine kwa kujipendeza mwenyewe.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.