Usikose Kupumzika Siku Yako ya Sabato
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Mariko 2:27,28 Akawaambia, Sabato ilifanyika kwa ajili ya mwanadamu, si mwanadamu kwa ajili ya sabato. Basi Mwana wa Adamu ndiye Bwana wa sabato pia.
Leo ni Jumamosi, siku ambayo Mungu aliagiza watu wake wapumzike. Kuanzia jioni Ijumaa hadi jioni Jumamosi ni siku iliyoitwa Sabato au Shabbat kwa lugha ya Kiebrania.
Neno lile, Shabbat, mara nyingi linatafsiriwa kama “mapumziko”. Lakini tafsiri sahihi zaidi in kuacha kufanya kazi, yaani kufunga mkataba ya shughuli za wiki zima kwa siku yake ya mwisho. Pia kinachonipendeza zaidi ni kwamba Sabato inaanza usiku wa Ijumaa.
Daima mimi nimeona kwamba jioni Ijumaa ni muda wa kipekee. Kwa kweli ni muda ninaopendelea katika wiki yote. Baada ya wiki nzima ya kazi ngumu lakini nzuri – yaani kazi katika huduma inaniletea furaha kubwa pamoja na kuridhika, lakini bado ni kazi ngumu – kwa kweli ni jambo bora kujitenga kidogo nayo, kuacha shughuli kwa muda na kujipatie angalau mapumziko.
Nafahamu kwamba si kila mtu anayo fursa ya kufanya hivyo, inategemeana na kazi yake na jinsi anavyopaswa kuajibika, lakini hata hivi kila mmoja wetu anahitaji angalau siku moja ya kupumzika au ikiwezekana, hata mbili.
Zamani, viongozi wa dini, kwa kuwa walikuwa manafiki, walimshambulia Yesu kwa sababu aliwaruhusu wanafunzi wake kuendelea njiani wakivunja masuke siku ya Sabato. Lakini Yesu aliwajibu hivi:
Mariko 2:27,28 Akawaambia, Sabato ilifanyika kwa ajili ya mwanadamu, si mwanadamu kwa ajili ya sabato. Basi Mwana wa Adamu ndiye Bwana wa sabato pia.
Ina maana, Mungu alitutengea siku moja ya kuacha kufanya kazi … kwa sababu gani? Ni kwa kutusaidia. Ni baraka kwetu.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.