Usisahau Kupumzika
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Mwanzo 2:1-3 Basi mbingu na nchi zikamalizika, na jeshi lake lote. Na siku ya saba Mungu alimaliza kazi yake yote aliyoifanya; akastarehe siku ya saba, akaacha kufanya kazi yake yote aliyoifanya. Mungu akaibarikia siku ya saba, akaitakasa kwa sababu katika siku hiyo Mungu alistarehe, akaacha kufanya kazi yake yote aliyoiumba na kuifanya.
Leo ni Jumapili ya pili ya mwaka huu mpya. Hatuendelei kukumbuka mambo kama hayo kadiri wiki zinavyoendelea kupita na sisi tukiendelea na shughuli zetu za kawaida. Bila shaka na wewe umeshaanza kusahau swala la “mwaka mpya” lakini ni muda mwafaka kutafakari leo kuhusu Jumapili ambazo ziko mbele yetu mwaka huu.
Jumapili ni siku isiyo ya kawaida katika wiki – sehemu nyingi duniani, ni siku ya kupumzika. Hapa kwetu, asubuhi Jumamosi, ni kama watu wote wametoka ndani ya magari yao. Lakini kesho yake, asubuhi Jumapili, mtu akiendesha gari lake kwenda kanisani, anakutana na magari machache sana.
Hailishi siku yako iliyopangwa kwa kupumzika ni siku gani – Jumapili au siku nyingine kufuatana na ratiba ya kazi yako – acha nikuulize swali hili: Je! Unapumzika kweli kweli siku ile ?
Nauliza hivi kwa sababu nimeshuhudia kwamba watu wengi wameacha kupumzika. Labda wamebaki nyumbani lakini ajira yao inatazamia wajibu barua pepe, na meseji na kupokea simu kana kwamba ni siku ya kazi kama kawaida. Sasa hali hiyo inaleta athari kwa njia nyingi – kwenye hisia za mtu, saikolojia na mahusiano yake na watu wengine. Ni hatari!
Mwanzo 2:1-3 Basi mbingu na nchi zikamalizika, na jeshi lake lote. Na siku ya saba Mungu alimaliza kazi yake yote aliyoifanya; akastarehe siku ya saba, akaacha kufanya kazi yake yote aliyoifanya. Mungu akaibarikia siku ya saba, akaitakasa kwa sababu katika siku hiyo Mungu alistarehe, akaacha kufanya kazi yake yote aliyoiumba na kuifanya.
Usisahau kupumzika!
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.