Usishangae
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Yohana 5:28,29 Msistaajabie maneno hayo; kwa maana saa yaja, ambayo watu wote waliomo makaburini wataisikia sauti yake. Nao watatoka; wale waliofanya mema kwa ufufuo wa uzima, na wale waliotenda mabaya kwa ufufuo wa hukumu.
Kwa kweli, hakuna kukwepa yanayoletwa na mauti. Mtu hapumui tena, moyo unasimama, damu haitembei tena, bongo inakufa na tangia muda ule, mwili unaanza kuoza. Yaani ni kikomo kabisa.
Ndiyo maana ahadi za Mungu ndani ya Yesu Kristo, Mwanae, zinaonekana kuwa hazituhusu kabisa, kwamba hazina uhusiano na hali halisi ya mazingira yetu hapa duniani. Kwa sababu ahadi kubwa kuliko zote ni kwamba kifo cha mwili, si mwisho. Ni chanzo cha maisha yetu mapya yatakaoendelea milele daima.
Tujaribu kukumbatia ukweli huo leo, tafadhali. Maiti ndani ya sanduku si mwisho, bali ni mwanzo. Kwa kuwa nimezika mama yangu mzee hivi karibuni, habari hii inanigusa sana. Baada ya kutazama jeneza yake kushushwa ndani ya shimo, ukweli huo ulitikisa mtazamo wangu na bado ninautafakari. Lakini Yesu alisema,
Yohana 5:28,29 Msistaajabie maneno hayo; kwa maana saa yaja, ambayo watu wote waliomo makaburini wataisikia sauti yake. Nao watatoka; wale waliofanya mema kwa ufufuo wa uzima, na wale waliotenda mabaya kwa ufufuo wa hukumu.
Ukweli ni kwamba kuna uzima wa milele kwa wote waliodhihirisha imani yao ya kweli ndani ya Yesu kwa matendo yao mema. Wataishi mbele zake milele na milele. Wasioidhihirisha imani hiyo, wao hawatakuwepo pale.
Msistaajabie maneno hayo; kwa maana saa yaja, ambayo watu wote waliomo makaburini wataisikia sauti yake. Kama umemwamini Yesu, kwa kweli siku ile itakuwa siku njema ya utukufu!
Usishangae wakati utasimama mbele zake katika utukufu wake milele daima.
Usistaajabu!
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.