Usitapanye Uhuru Wako
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Wagalatia 5:13 Maana ninyi, ndugu, mliitwa mpate uhuru; lakini uhuru wenu usiwe sababu ya kuufuata mwili, bali tumikianeni kwa upendo.
Haya, ni tarehe 4 ya mwezi Julai. Hata uwe unaishi wapi kwenye dunia yetu, huwezi kukosa kufahamu kwamba huko Marekani ambayo ni nchi tajiri kuliko zote, ni siku ya kuadhimisha uhuru wao.
Kujitawala kunahusu uhuru, lakini bila kueleza kwa undani zaidi, ni hakika kwamba utajiri wa Marekani ulijengwa juu ya msingi wa utumwa; ule uonevu mbaya unaofuatana kabila na rangi ya ngozi.
Tunamshukuru Mungu kwamba leo haupo tena. Lakini sijui kama ulifahamu kwamba kuna nchi ndogo katika Afrika Magharibi, iitwayo Liberia yenye idadi ya wananchi milioni tano hivi. Ni nchi iliyoanzishwa mwaka 1850 na watumwa waliowekwa huru kutoka Marekani. Ndio maana bendera yao inafanana sana na bendera ya Marekani, ila ina nyota moja tu badala ya hamsini.
Lakini kwa mwisho wa karne iliyopita, mapinduzi ya jeshi na utawala wa kikatili wa dikteta Charles Taylor vilisababisha vita ya wenyewe kwa wenyewe na ukandamizaji mbaya. Sasa mtu angefikiri kwamba watumwa waliowekwa huru wangethamini kuishi katika amani na uhuru kama vile hata jina la nchi yao – Liberia – linaloashiria!
Lakini wala!. Na bila kukupa somo ndefu la historia, lengo la masimulizi haya ni kwamba, sisi binadamu tuna tabia ya ajabu kutapanya uhuru wetu; yaani kushindwa kutunza kitu chenye thamani kubwa.
Wagalatia 5:13 Maana ninyi, ndugu, mliitwa mpate uhuru; lakini uhuru wenu usiwe sababu ya kuufuata mwili, bali tumikianeni kwa upendo.
Onyo hili si kwa ajili ya watu wa Marekani au Liberia tu, bali ni kwa ajili ya sisi sote kwasababu tukianza kufanya yanayopendeza asili yetu ya dhambi, tutatapanya uhuru tuliopewa na Mungu.
Bali tumikianeni kwa upendo.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.