... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Usiufiche Msalaba

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Matendo 4:11,12 Yeye ndiye jiwe lile lililodharauliwa na ninyi waashi, nalo limewekwa kuwa jiwe kuu la pembeni. Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo.

Listen to the radio broadcast of

Usiufiche Msalaba


Download audio file

Kuna sababu moja inayonisukuma kufanya ninayoyafanya, inayoniamsha kila siku nitoke kitandani.  Ni shauku endelevu kuwaambia watu wengi iwezekanavyo habari za Yesu.  Kinachonihuzunisha ni kwamba wengine hawataki kuzijua.

Kila mtu aliyepokea neema ya ajabu ya Mungu ndani ya Yesu, lazima atapenda watu wengine waipate na wao; wajue upendo wa Mungu ndani ya Yesu Kristo.

Lakini, sijui kama umeshagundua, wengi hawataki kujua.  Kwa hiyo mtu anaweza akashawishika agoshie kidogo Injili, iwe mwororo na kuacha kuongea habari ya dhambi na adhabu na msamaha uliomo ndani ya Kristo.  Unajua, hiki ndicho kinachowakwaza.  Na ndivyo ilivyokuwa tangu mwanzo. 

Katika hotuba yake, akiwahubiri wale wale waliopaza sauti Yesu auawe, wale walioomba asulubiwe, Mtume Petro aliweza kusema yafuatayo:

Matendo 4:11,12  Yeye ndiye jiwe lile lililodharauliwa na ninyi waashi, nalo limewekwa kuwa jiwe kuu la pembeni.  Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo.

Watu walianza kumkataa Yesu mapema sana, tangu mwanzo.  Lakini jibu si kugoshia Injili, hapana.

Kama vile Charles Spurgeon aliwahi kusema:  Ndugu zangu wapendwa, usijaribu kufanya Injili iwe tamu kwa fikra za watu wanaojali mambo ya mwili tu.  Usifiche shutumu la msalaba, la sivyo unaweza kubatilisha matokeo yake mazuri.  Makona yote ya Injili yanaipa nguvu; kujaribu kuyapunguza ni kuinyima uweza wake.  Kupunguza ukali wake hakutaongeza nguvu zake, bali kutasababisha ife.

Watu wataendelea kukataa Habari Njema ya Yesu, lakini kamwe usiigoshie kwa sababu kufanya hivyo itaondoa kabisa nguvu zake. 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.


We use cookies to improve your browsing experience, analyse site traffic & personalise content, but we do not track you when you leave this site. To find out how we utilise & protect your data, check out our "Privacy Policy".

Privacy Policy