Usiwe Mvivu
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Mithali 12:27 Mtu mvivu hapiki mawindo yake; bali mwenye bidii anazo mali za thamani.
Je! Ni lini haja ya kupumzika inaweza kuwa udhuru wa uvivu? Sisi sote tunahitaji kupumzika baada ya kazi ngumu, lakini ni vigumu kutofautisha mapumziko halali na moyo wa ulegevu unaompelekea mtu kuwa mvivu.
Kuna wakati watu wananiuliza kwa nini ninafanya kazi kwa nguvu. Jibu ni rahisi. Kila siku watu wasiohesabika wanakufa na kuingia umilele bila Kristo. Mungu ameniita niwaambie habari za Yesu, kwa hiyo kuna umuhimu unaonisukuma kuwa na haraka kutimiza kazi yangu.
Kuna wakati natumika sana kuliko inavyotakiwa, labda wewe pia unaweza kufanya hivyo. Na hata kama kwa asili yangu mimi si mvivu, nikisema ukweli, mara kwa mara kuna kishawishi kinachonijia cha kupunguza kasi na kulegeza na kustarehe.
Kufanya hivyo ni aina ya mapumziko, lakini mtu akiendelea tu katika starehe, inabadilika kuwa uvivu mtupu. Mfalme Sulemani, miaka elfu tatu iliyopita alitamka wazi akisema:
Mithali 12:27 Mtu mvivu hapiki mawindo yake; bali mwenye bidii anazo mali za thamani.
Mimi binafsi, si kwamba natafuta mali. Ninachotaka ni kukutia moyo katika safari yako ya imani; kuona watu wengine wengi wasiohesabika kufikia ujuzi wa Yesu uokoao.
Lakini haijalishi tuna tabia gani au jinsi tulivyoumbwa, kila mara kunaweza kutokea jaribu la kuanza kuwa mvivu. Kuna mfia dini, mchungaji wa China aitwaye Watchman Nee alieleza hivi:
“Mara nyingi watu wanasema kwamba kupumzika ni uvivu tu. Lakini mwili unahitaji kupumzishwa kama vile hata mawazo yetu na roho pia. Lakini kamwe tusipumzike kutokana na uvivu unaoibuka kwenye asili yetu ya uovu ulio ndani yetu. Mara nyingi uvivu na kuogopa kazi ngumu vinaunganika pamoja kutumia udhuru wa kusema mwili umechoka.”
Mtu mvivu hapiki mawindo yake; bali mwenye bidii anazo mali za thamani.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.