Ustaarabu Unao-oza
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
2 Petro 3:3,4 Mkijua kwanza neno hili ya kwamba katika siku za mwisho watakuja na dhihaka zao watu wenye kudhihaki, wafuatao tamaa zao wenyewe, na kusema, Iko wapi ahadi ile ya kuja kwake? Kwa maana, tangu hapo babu zetu walipolala, vitu vyote vinakaa hali iyo hiyo, tangu mwanzo wa kuumbwa.
Sijui kama umechoshwa na kuangalia au kusoma au kusikiliza habari za dunia. Taarifa za ulimwengu huwa zinanichosha. Mtu akijituliza kidogo ili achunguze vizuri, anaona kama ustaarabu wa kibinadamu umepinduliwa na watu wanabaki wakibishana na kutenda yasiyofaa kabisa.
Labda kidogo inaonekana kama nimekosa busara … lakini inafaa sana kuendelea kujua ni nini kinaendelea ulimwenguni. Lakini taarifa za habari zimebaki kuwa kelele za ukosoaji tu.
Teana isitoshe kuna mambo hayaeleweki kabisa: Shule zinapiga marufuku kutumia neno “mama” au “baba” kwasababu yanawakwaza wasiojua jinsia zao. Wanaume wanavaa kama wanawake huku wakishindana kwenye michezo ya akina mama na kupata ushindi. Watu wanapongeza sheria zinazoruhusu utoaji mimba.
Lakini mtu akithubutu kusimama kidete na kusema kwamba wanayoyafanya hayafai kabisa, tena hayaeleweki, mara moja wengine wanajaribu kumwangusha na kumnyamanzisha.
2 Petro 3:3,4 Mkijua kwanza neno hili ya kwamba katika siku za mwisho watakuja na dhihaka zao watu wenye kudhihaki, wafuatao tamaa zao wenyewe, na kusema, Iko wapi ahadi ile ya kuja kwake? Kwa maana, tangu hapo babu zetu walipolala, vitu vyote vinakaa hali iyo hiyo, tangu mwanzo wa kuumbwa.
Maneno hayo yaliandikwa miaka 2000 iliyopita. Hakuna mapya. Kuna mwanafalsafa aliyekuwa mwanatheolojia pia aitwaye GK Chesterton alisema hivi: Ustaarabu wote ulioinuliwa huwa unaoza kwa kusahau mambo dhahiri. Hayo ndiyo yanayotokea siku hizi.
Je!, Unamwamini Yesu? Usishiriki katika uharibifu huo. Usisahau yaliyo dhahiri. Sote ni wenye dhambi. Yesu alikufa ili tusamehewe, halafu alifufuka ili maisha yetu yabadilishwe.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.