... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Kazi Yako na Kazi Yangu

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Yohana 3:17 Maana Mungu hakumtuma Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye.

Listen to the radio broadcast of

Kazi Yako na Kazi Yangu


Download audio file

Sijui unaonaje, lakini nikitazama mambo yanayotendeka ulimwenguni – mienendo ya watu na muelekeo wa mambo – ninajiuliza, Dunia hii mbona inapelekwa Jehanamu bila mtu kuizuia? 

Ni rahisi kukatishwa tamaa, kuhukumu “wenye dhambi walioko huko” sindiyo?  Tunataka kusimama juu kwenye kilele cha mlima na kulalamikia kundi hili, kulaani kundi lile tukimwomba Mungu awanyamazishe. 

Eeh, najua kama nimetumia maneno makali lakini ndivyo tunavyohisi mara nyingi, si kweli?  Maana wakristo wengi wanajiona kuwa wanafunzi wa Yesu Kristo lakini sio, ni wakosoaji wa hali ya juu wakihukumu watu wengine na kubishana nao.  Hali hiyo haipendezi.  Wengine wanajitenga kabisa na “wenye dhambi walioko huko” – kana kwamba;- wao ni wazuri kuzidi watu wote. 

Lakini, kusema ukweli, hii ni kazi yetu sote?  Je!,  Kristo ametuagiza kuishi hivyo? 

Yohana 3:17  Maana Mungu hakumtuma Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye. 

Ebu tutafakari maneno hayo kidogo.  Kama Yesu hakuja ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, nadhani si kazi yetu kuuhukumu.  Na kama Yesu alikuja kuokoa ulimwengu … basi hiyo ndio kazi ambayo na sisi pia tungeishugulikia. 

Ni rahisi kunung’unika, tukilalamikia kila kitu au kila mtu!  Lakini sidhani kama ndio sababu ya Mungu kuusukuma  moyo wako na moyo wangu ufanye kazi kawaida Kazi yetu si kuhukumu ulimwengu,  Kazi yetu ni kujaribu kuuokoa . 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.