... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Mkakati Mzuri, Lakini …

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Mathayo 13:23 Naye aliyepandwa penye udongo mzuri, huyo ndiye alisikiaye lile neno, na kuelewa nalo; yeye ndiye azaaye matunda, huyu mia, na huyu sitini, na huyu thelathini.

Listen to the radio broadcast of

Mkakati Mzuri, Lakini …


Download audio file

Kanisa kubwa la Westminster Abbey huko London limekuwa sehemu ya kutawaza wafalme na malkia wote wa Waingereza tangu mwaka wa 1066.  Wakati ule jengo hili nzuri lilikuwa bado halijakamilika kama ilivyo leo, lakini chanzo chake kilikuwepo karibia miaka 1000.

Tangu wakati ule, ni majengo mangapi makubwa ya makanisa yameshajengwa ili yazidi yale yaliyotangulia?  Siku hizi, tunajenga majengo makubwa mno ya watu maelfu yakiwa na menejimenti za kisasa, na mikakati mikubwa pamoja na mbinu za kushawishi watu kiujanja. 

Siseme kwamba hayo yote ni mabaya!, hapana.  Pia hakuna ubaya kwako au kwangu kwa kuwa na mipango pamoja na mikakati ya kumtumikia Mungu.  Lakini kama vile Winston Churchill alivyosema, “Hata kama mkakati unaweza kuwa mzuri kiasi gani, bado ni lazima uchunguzwe ili kuona kama unaweza kuleta matokeo yoyote.” 

Bila shaka umeshasikia namna Yesu alivyosema kwamba makusudi yetu mema yanaweza kufaulu au kufeli.  Katika mioyo ya watu baadhi Neno la Mungu linaangukia kwenye udongo mgumu na haliwezi kuanza kuota mizizi.  Kwa wengine, linaangukia sehemu isiyokuwa na udongo mwingi na hata likiota linakufa kwa hari ya jua kali.  Pengine Neno linasongwa na majani mabaya na miiba – yaani mahangaiko ya ulimwengu huu.  Halafu mwishowe anatwambia kinachotakiwa: 

Mathayo 13:23  Naye aliyepandwa penye udongo mzuri, huyo ndiye alisikiaye lile neno, na kuelewa nalo; yeye ndiye azaaye matunda, huyu mia, na huyu sitini, na huyu thelathini. 

Ina maana kwamba, Neno la Mungu linaota mizizi ndani ya mioyo yetu, lengo ni kwamba lizae matunda.  Tumekusudiwa kuleta mabadiliko duniani.  Ni vizuri kuwa na mikakati mikubwa, lakini kumfuata Yesu si swala la kuwa na mkakati mzuri hasa, bali linahusu matokeo mazuri, yaani kuzaa matunda mengi. 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.