... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Ustadi wa Kutokufanya Chochote

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Mariko 6:30-31 Na mitume wakakusanyika mbele ya Yesu; wakampa habari za mambo yote walioyoyafanya, na mambo yote waliyoyafundisha. Akawaambia, Njoni ninyi peke yenu kwa faragha, mahali pasipokuwa na watu, mkapumzike kidogo. Kwa sababu walikuwako watu wengi, wakija, wakienda, hata haikuwapo nafasi ya kula.

Listen to the radio broadcast of

Ustadi wa Kutokufanya Chochote


Download audio file

Acha nikuulize, je!, Kwa kipimo cha moja hadi kumi, wewe uko kwenye kiwango kipi. Je! Wewe ni mmojawapo wa wale wakiulizwa, “Vipi  Mambo yanakwendaje?”  unajibu hivi, “Niko bize, bize, bize, kama kawaida”!

Nafahamu kwamba si kila mtu yuko bize kupita kiasi.  Wengine, hasa wale ambao wana kipaji cha kuwa watuninaopenda kuwaita “wataratibu”, kwa kweli maisha yao ni ya utulivu. Lakini wengine wengi, maisha mara nyingi ni yenye msisimko na shughuli nyingi hata vurugu, watu wakishindwa kutekeleza na kutimiza wajibu wao katika kazi na hata katika maisha yao binafsi. 

Kwa hiyo ni jambo lenye tafakari kuelewa kwamba, zamani, hata kwa Yesu, maisha yalikuwa hivi mara nyingi.  Ni kweli yeye hakusumbuliwa na mtandao unaosisimua na kumshtua mtu masaa ishirini na nne kila siku ya wiki kama ilivyo leo, lakini hata hivyo, alikuwa mtu maarufu.  Alikuwa kama mwimbaji mashuhuri. Yaani, alipokaribia kijiji fulani, wanakijiji wote waliacha shughuli zao na kumwendea ili waweze kumsikia akihubiri na kushuhudia miujiza yake. 

Umati wa watu walimsonga. Ilimwia vigumu kuongoza wafuasi wake, tena isitoshe, hakusafiri kwa gari lenye AC, ilimlazimu atembee kwa miguu – kwenye baridi na mvua na siku zingine kwenye jua kali. 

Mariko 6:30-31  Na mitume wakakusanyika mbele ya Yesu; wakampa habari za mambo yote walioyoyafanya, na mambo yote waliyoyafundisha.  Akawaambia, Njoni ninyi peke yenu kwa faragha, mahali pasipokuwa na watu, mkapumzike kidogo.  Kwa sababu walikuwako watu wengi, wakija, wakienda, hata haikuwapo nafasi ya kula. 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.


We use cookies to improve your browsing experience, analyse site traffic & personalise content, but we do not track you when you leave this site. To find out how we utilise & protect your data, check out our "Privacy Policy".

Privacy Policy