... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Tumia Akili Zako

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Waebrania 11:7 Kwa imani Nuhu akiisha kuonywa na Mungu katika habari za mambo yasiyoonekana bado, kwa jinsi alivyomcha Mungu, aliunda safina, apate kuokoa nyumba yake. Na hivyo akauhukumu makosa ulimwengu, akawa mrithi wa haki ipatikanayo kwa imani.

Listen to the radio broadcast of

Tumia Akili Zako


Download audio file

Huwa kuna mvutano mkubwa kwenye maisha yetu katika yale Mungu anatutaka. Yaani ni vigumu kujua tutumie imani kiasi gani kufuata mawazo ya ajabu ajabu yanayotujia kichwani na kujua ni kiwango gani cha busara chatupasa kutumia kwa kukamilisha mipango yetu.

Ningefurahi kusikia kama na wewe una changamoto kama hiyo mara kwa mara; hii ingenionyesha kwamba unaishi kwa imani mahali ambapo kama Mungu asingekuonekania basi mambo yangekuharibikia kabisa. Yaani ni sehemu nzuri kuishi kwasababu inatulazimisha kumtegemea Mungu zaidi. 

Sasa tukiongea swala la mawazo ya ajabu ajabu, ebu fikiria habari ya Nuhu kuunda safina mahali ambapo hakuna bahari, si jambo la ajabu kwelikweli.  Ilimchukua miaka mingi sana, alitumia pesa nyingi, kazi ngumu sana ya kuchosha, watu wengine walikuwa wanamdhihaki mzee yule Nuhu, wakisema amerukwa na akili.  Lakini alistahimili … 

Waebrania 11:7  Kwa imani Nuhu akiisha kuonywa na Mungu katika habari za mambo yasiyoonekana bado, kwa jinsi alivyomcha Mungu, aliunda safina, apate kuokoa nyumba yake.  Na hivyo akauhukumu makosa ulimwengu, akawa mrithi wa haki ipatikanayo kwa imani. 

Ni kweli kabisa, Nuhu aliunda safina kwa imani, lakini ilibidi afuate ramani na kutafuta vifaa na kutumia vipimo maalum.  Kulitumika uhandisi fulani wa meli. Useremala ulitumika. Kwa mafupi, bila kuwa na mipangilio ni rahisi kusema swala kuunda safina lisingewezekana. 

Ninachotaka kusema ni kwamba, kufikiri ni sehemu muhimu sana kwenye safari yetu ya imani. Si kwamba mtu anachukua moja na kuacha nyingine, hapana. Ni yote mawili. Fuata kabisa kwa moyo wako wote wito ule wa Mungu usioeleweka.  Ndiyo, tembea kwa imani.  Lakini tumia akili zako pia. 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.