Utamfananisha na Nani?
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Isaya 46:5,6 Mtanifananisha na nani, na kunisawazisha naye, na kunilinganisha naye, ili tuwe sawasawa? Watu wamwagao dhahabu kutoka mfukoni, na kupima fedha katika mizani, huajiri mfua dhahabu, akaifanya mungu; huanguka, naam, huabudu.
Leo ni siku ya Jumapili tena. Kwa wamoja, ni mwisho wa wiki, kwa wengine ni mwanzo wa wiki inayofuata. Haijalishi uko kwenye kundi gani, tusherehekee kwa pamoja Jumapili. Tuone fahari katika utukufu wa Mungu na kumstaajabia.
Siku ya leo ilikusudiwa kuwa siku ya mapumziko. Ndiyo, siku ya kustarehe na kufanya mambo yanayokupendeza, lakini hasa kuweka mawazo yetu juu ya Mungu anayetupenda kuliko jinsi tungeelezea; siku ya kuinua macho yetu kuangalia mambo ya mbinguni.
Kwa sababu siku zingine za wiki, mara nyingi vichwa vyetu vinaangalia chini kwa kukabiliana na maisha – mambo mazuri, mabaya, na yasiyopendeza. Mazingira ya maisha ya kila siku mara nyingi yanafumba macho yetu tusiweze kumtazama Mungu – tusipoweza kumwona jinsi alivyo na yale awezayo kuyafanya. Muda umewadia kuinua macho yako kumwangalia Mungu mwenyewe. Ni muda mzuri kutulia na kuelewa kwamba yeye ndiye Mungu.
Isaya 46:5,6 Mtanifananisha na nani, na kunisawazisha naye, na kunilinganisha naye, ili tuwe sawasawa? Watu wamwagao dhahabu kutoka mfukoni, na kupima fedha katika mizani, huajiri mfua dhahabu, akaifanya mungu; huanguka, naam, huabudu.
Hakuna kitu duniani, hata kama ni fedha na dhahabu au mungu mwingine awaye yote ambaye mtu angejitengenezea katika ulimwengu huu unaoendeshwa na mafanikio na kupata mali … hakuna hata mmoja anayoweza kufananishwa na upendo wa Mungu wenye wangavu aina nyingi, Mungu aliyetangazwa na manabii, na watunga zaburi wakamwimbia. Hakuna.
Mtanifananisha na nani, na kunisawazisha naye, na kunilinganisha naye, ili tuwe sawasawa?
Na Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.