... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Utengano Unaofisha Umoja

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Warumi 15:5,6 Na Mungu mwenye saburi na faraja awajalie kunia mamoja ninyi kwa ninyi, kwa mfano wa Kristo Yesu; ili kwa moyo mmoja na kwa kinywa kimoja mpate kumtukuza Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo. Kwa hiyo mkaribishane ninyi kwa ninyi, kama naye Kristo alivyotukaribisha, ili Mungu atukuzwe.

Listen to the radio broadcast of

Utengano Unaofisha Umoja


Download audio file

Kinachokera zaidi ni wakati wenye mamlaka wanachezea mambo ya siasa badala ya kujitolea kwa faida ya watu ambao wanawatawala, wakishutumiana na kuwindana kwa kugombania vyeo.

Tumeshashuhudia hayo mara nyingi.  Kutokuwa na umoja ni dalili kwamba chama fulani cha siasi kinaenda kufa kabisa.  Hawawezi kutazamia kushinda katika uchaguzi kama wanagombana wao kwa wao. 

Lakini hali hiyo mbaya haitokei kwenye siasa tu.  Hata kwenye vikundi vya michezo au shirika la wakazi wa eneo fulani hua inatokea.  Mimi mwenyewe nimehusishwa katika maswala kama hayo na kwa kweli nimechukizwa mno na jinsi watu wanavyokorofishana.  

Cha kuhuzunisha pia, unaweza kushuhudia hali hiyo mbaya hata ndani ya kanisa, ushirika ambao unaotakiwa umwakilishe Kristo mbele ya ulimwengu uliopotea na kuumia.  Miaka kadha iliyopita, nilihudhuria kanisa fulani (lakini si kwa muda mrefu, hapana) ambalo viongozi walifikiri ni wajibu wao ni kukosoa hadharani madhehebu mengine au mifumo mingine isiyoendana na ya kwao.  Jamani!  Lakini sikiliza yafuatayo: 

Warumi 15:5-7 Na Mungu mwenye saburi na faraja awajalie kunia mamoja ninyi kwa ninyi, kwa mfano wa Kristo Yesu; ili kwa moyo mmoja na kwa kinywa kimoja mpate kumtukuza Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo. Kwa hiyo mkaribishane ninyi kwa ninyi, kama naye Kristo alivyotukaribisha, ili Mungu atukuzwe.

Siyo kazi yetu kushindana kwa maswala ya kiteolojia au hoja zinazohusu kanisa.  Wajibu wetu kwa pamoja ni kumletea Mungu utukufu. 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.


We use cookies to improve your browsing experience, analyse site traffic & personalise content, but we do not track you when you leave this site. To find out how we utilise & protect your data, check out our "Privacy Policy".

Privacy Policy