... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Uwe Makini kuchagua Rafiki Zako

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Mithali 13:20 Enenda pamoja na wenye hekima, nawe utakuwa na hekima; bali rafiki wa wapumbavu ataumia.

Listen to the radio broadcast of

Uwe Makini kuchagua Rafiki Zako


Download audio file

Je!  Washauri wako wa karibu ni akina nani?  Kama umeshafunga ndoa, naamini kwamba mshauri wako wa kwanza ni mwenzako.  Lakini wengine walio karibu nawe, vipi? Je!  Wanapaswa kuwa rafiki wa karibu kweli kweli?  Haya ni maswali ya msingi kwa sababu, watu wale wanaweza kuboresha maisha yako au wanaweza kuyaharibu kabisa.

Sisemi kwamba tujaribu kutafuta kuwa na marafiki waliokamilika kabisa. Sehemu kubwa ya kazi ya mfuasi wa Kristo ni kutangaza upendo wake na Habari Njema ya Yesu kwa watu ambao hawajamjua; kuwaonekania kwa huruma wale wanaoumia. 

Watu kama hawa, hawakukamilika hata kidogo, lakini lazima tuwakaribie kama vile Yesu aliwakaribia watu waliotengwa na jamii.  Lakini tuwe na tahadhari.  Kuwa karibu sana na watu wasiofaa kunaweza kukuharibia maisha. 

Mithali 13:20  Enenda pamoja na wenye hekima, nawe utakuwa na hekima; bali rafiki wa wapumbavu ataumia. 

Dhana hii ya kuenenda pamoja na wenye hekima ingesababisha mtu ajiulize, Ni akina nani ambao amewaruhusu kuwa rafiki wa karibu maishani mwake?  Ni wepi anaojaribu kuwaiga?  Ni wepi ambao anawaomba ushauri? 

Lakini pia, dhana ya kuwa rafiki ya wapumbavu inaeleza jinsi mtu anaweza kuwaruhusu wasiofaa kumshawishi na kumwongoza. 

Acha nikuulize tena, je!  Ni akina nani umeruhusa kuwa washauri wako wa karibu?  Ebu jaribu katika mawazo yako kumwangalia kila mmoja sura yake na kujiuliza, je!  Mtu huyu ni mwenye hekima au ni mpumbavu?  Kwa sababu … 

Enenda pamoja na wenye hekima, nawe utakuwa na hekima; bali rafiki wa wapumbavu ataumia. 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.


We use cookies to improve your browsing experience, analyse site traffic & personalise content, but we do not track you when you leave this site. To find out how we utilise & protect your data, check out our "Privacy Policy".

Privacy Policy