Uwe Mtakatifu
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
1 Petro 1:15,16 Bali kama yeye aliyewaita alivyo mtakatifu, ninyi nanyi iweni watakatifu katika mwenendo wenu wote; kwa maana imeandikwa, Mtakuwa watakatifu kwa kuwa mimi ni mtakatifu.
Ninashangaa nikiangalia maajabu wanariadha wenye vipaji wanavyofaulu kutenda, si kwa sababu ya vipaji vyao tu, lakini kwa sababu ya jitihada zao pia pamoja na mazoezi magumu wanaoyapitia.
Mwanadamu wa kwanza aliyeweza kukimbia maili moja chini ya dakika nne alikuwa Roger Bannister. Mai 6, 1954, mwanafunzi yule aliyekuwa na umri wa miaka 25, akisoma kuwa mganga kwenye Chuo Kikuu cha Oxford, alifika kwenye uwanja kwa mashindano yaliyotokea kila mwaka.
Mazingira yalitatanisha. Kulikuwa upepo mkali ulivuma pembeni ya uwanja wakati mashindano ya maili moja yalitaka kuanza. Msimamizi alipiga bastola ya kuanza halafu baada ya dakika tatu na sekundi hamsini na tisa na nukta nne, Bannister alipita mstari wa kumaliza. Wahudhuriaji walipiga makofi na vigelele wakati spidi yake ilitangazwa rasmi. Alikuwa ni mtu asiye wa kawaida, na tukio lenyewe lilikuwa si la kawaida.
Sijui kama umewahi kujiona kuwa mtu asiye wa kawaida, aliyekusudiwa kupitia matukio yasiyo ya kawaida. Labda hujajiona hivyo. Labda utashangaa kusikia kwamba Mungu anakuona kuwa mtu asiye wa kawaida. Wewe ni mtu wa kipekee, unapendwa sana, umetakaswa kwa ajili ya lengo maalum.
Lakini mara nyingi tunatimiza wajibu wetu wa kila siku tu na kukosa kuona mipango yake Mungu. Je! Bannister angeshinda kwa kukimbia maili moja chini ya dakika nne kama angekaa tu kwenye baa badala ya kwenda nje na kufanya mazoezi kwenye uwanja wa mashindano?
Ndiyo maana Mungu alitamka hivi:
1 Petro 1:15,16 Bali kama yeye aliyewaita alivyo mtakatifu, ninyi nanyi iweni watakatifu katika mwenendo wenu wote; kwa maana imeandikwa, Mtakuwa watakatifu kwa kuwa mimi ni mtakatifu.
Kuwa mtu wa kipekee machoni pa Mungu ni sawa, lakini lazima tuishie maono hayo. Uwe mtakatifu kwa kuwa Bwana Mungu wako ni mtakatifu.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.