Uwe Mwenye Upendo
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Yakobo 2:8,9 Lakini mkiitimiza ile sheria ya kifalme kama ilivyoandikwa, Mpende jirani yako kama nafsi yako, mwatenda vema. Bali mkiwapendelea watu, mwafanya dhambi na kuhukumiwa na sheria kuwa wakosaji.
Sasa, ni mara ngapi umehukumu na kutathmini kitabu fulani kwa kuangalia jalada Lake tu? Sitaki kukuhukumu, lakini nadhani kama ukisema ukweli, sio mara chache, au? Sisi sote tuko hivi. Sote tunahukumu kwa haraka.
Tuchimbe zaidi katika swala hilo. Je! Ukikutana na mtu aliyenenepa kupita kiasi, mara moja unamwonaje ukimlinganisha na mwingine ambaye ni wa kawaida? Au mtu mwenye sura nzuri na mwingine ambaye hafikii kiwango kilichopangwa na jamii kwa jinsi urembo unaopaswa kuwa? Au kulinganisha mtu mwema mwenye fadhili na mwingine?
Nafikiri tuko pamoja. Sisi sote tunatathmini vitabu kwa kuangalia jalada la nje tu. Na mara nyingi, bila hata kufikiria tunajiosha kwa tendo hilo. Ndivyo ilivyo. Mmmh!.
Yakobo 2:8,9 Lakini mkiitimiza ile sheria ya kifalme kama ilivyoandikwa, Mpende jirani yako kama nafsi yako, mwatenda vema. Bali mkiwapendelea watu, mwafanya dhambi na kuhukumiwa na sheria kuwa wakosaji.
Jamani!, Labda hujafikiria sana kama ilivyoelezwa katika mistari hii. Yaani si jambo dogo mbele za Mungu, kwasababu kila mtu, haijalishi kama wanatupendeza au la, kila mtu aliumbwa kwa sura ya Mungu; kila mtu anapendwa na Mungu sawa sawa na jinsi Mungu anavyotupenda!
Kwahiyo kipimo kinachotupasa kutumia kwa kuwatendea wengine, wanaopendeza na wasiopendeza, ni hiki kimoja: Mpende jirani yako kama nafsi yako. Basi.
Rafiki yangu, kujua na kufanya hivyo, si jambo gumu kama vile sayansi ya hali ya juu inayoweza kupeleka roketi huko mwezini, hapana.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.