... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Je!, Umechoka?

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Onea Wengine Huruma Yakobo 2:13 Maana hukumu haina huruma kwake yeye asiyeona huruma. Huruma hujitukuza juu ya hukumu.

Listen to the radio broadcast of

Je!, Umechoka?


Download audio file

Sijui ukoje, lakini mimi ninamwamini Yesu.  Kwahiyo, siku ile ya hukumu ambayo haina budi kutufikia sote, najua kwamba nitahurumiwa na Mungu.  Lakini kuna wazo moja linalotisha:  Itakuaje nisipoipata ile huruma?  Itakuaje usipoipata na wewe?

Huruma ya Mungu haieleweki mpaka pale mtu aelewe kwanza ghadhabu ya Mungu.  Mahakamani, mhalifu akionekana kwamba ametenda kosa kweli na ni la jinai, tunatazamia hakimu kutokumwonyesha huruma wakati wa hukumu, si kweli?  Ni kwa sababu tumeumbwa kwa sura ya Mungu, tukiwa na nia ya kuona haki itendeke.  Kwahiyo tusifute habari za haki ya Mungu na gadhabu yake hat kama zinatuchukiza. 

Lakini moyo wa Mungu ni moyo wa upendo, una neema na huruma.  Ndiyo maana alimtuma Yesu kufa pale msalabani kwa ajili ya wewe na mimi, ili atimize masharti ya haki yake.  Ndio maana natazamia kwa kupitia imani yangu ndani ya Yesu kupokea huruma zake siku ile ya kutoa hesabu. 

Lakini je! Kuna jambo lolote lile ambalo lingenitoa kwenye reli ya huruma ile? 

Yakobo 2:13  Maana hukumu haina huruma kwake yeye asiyeona huruma.  Huruma hujitukuza juu ya hukumu. 

Usinilaumu mimi. Mimi ni mjumbe tu.  Maneno hayo yanatoka moja kwa moja ndani ya Neno la Mungu, yakiwa mhutasari sahihi wa mfano jinsi Yesu alivyotoa mfano kuhusu mfanyakazi mmoja aliyesamehewa na bwana wake deni kubwa mno, halafu akamshurutisha mfanyakazi mwenzake kumlipa deni ndogo sana.  Wakati bwana wake anapata habari hizo, kweli ghadhabu yake haikuweza kutulizwa hata kidogo. 

Hukumu haina huruma kwake yeye asiyeona huruma. 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.