Uwe na Huruma
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Mariko 6:34 Naye aliposhuka mashuani, akaona mkutano mkuu, akawa hurumia; kwa sababu walikuwa kama kondoo wasio na mchungaji; akaanza kuwafundisha mambo mengi.
Ulimwengu huu tunamoishi unamashindano mengi sana. Watu wanapiga kelele wakigombania vyeo, ajira, kuinuliwa, kujulikana n.k. Kwa kweli ni ulimwengu wa vurugu kwa jinsi watu wanavyoshindania mambo hayo.
Ni kweli, si kila mtu anayegombania hivyo. Kuna watu wengi wapole sana. Lakini mazingira yetu na utamaduni wetu vinatulazimisha mara kwa mara kushindana sana ilitupige hatua mbeleni; hata kuwakanyaga watu wengine ili tufike mahali tunapofikiri panapotustahili.
Isitoshe, tukizidi kwenda mbali na hali halisi ya maisha kwa sababu tunachukua muda mrefu sana kutazama skrini za simuzetu za mikononi, tunabaki kuwa watu ambao wameacha ubinadamu wao katika uhusiano wetu na watu wengine. Dhana ya kuhurumiana, kumbe imeishakuwa kama wazo la kigeni sasa. Lakini siyo hivyo kwa Yesu:
Mariko 6:34 Naye aliposhuka mashuani, akaona mkutano mkuu, akawahurumia; kwasababu walikuwa kama kondoo wasio na mchungaji; akaanza kuwafundisha mambo mengi.
Wengi wao waliokuwemo katika umati ule mkubwa wa watu ni wao wenyewe ambao baada ya miezi kadhaa wangepiga kelele na kusema, “Na asulubiwe, na asulubiwe!” Lakini hata hivi, Yesu aliwahurumia. Aliwatambua kuwa kama kondoo wasio na mchungaji, watu ambao walipotoshwa na viongozi wao wa dini.
Nadhani hakuna kitu ambacho kinachukiza sana kuliko kumwona mwanadamu asiye na huruma.
Ndiyo, kuna watu baadhi wanaweza mara kwa mara kukutendea visivyo. Wanaweza hata kukutendea jeuri.
Lakini uwe kama Yesu. Uwahurumie.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.