... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Uwe na Msimamo

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Warumi 14:7,8 Kwa sababu hakuna mtu miongoni mwetu aishiye kwa nafsi yake, wala hakuna afaye kwa nafsi yake. Kwa maana kama tukiishi, twaishi kwa Bwana, au kama tukifa, twafa kwa Bwana. Basi kama tukiishi au kama tukifa, tu mali ya Bwana.

Listen to the radio broadcast of

Uwe na Msimamo


Download audio file

Sijui kama utaniruhusu nikuulize swali leo?  Hivi, ni kipi kinasababisha imani yako ndani ya Yesu kumeguka?  Ni shida gani, au mashaka gani, au ni matatizo gani, au hofu gani, au mahusiano gani ambayo yanajaribu kubomoa imani yako?

Daima, mtu hawezi kukosa angalau kitu kimoja chakumsumbua, si kweli?  Kuna wakati mtu anachoshwa sana na kuwa na mashaka kwamba labda imani yake ndani ya Yesu haileti mabadiliko yoyote maishani mwake, sembuse katika maisha ya wanaomzunguka.  Hofu na mashaka vinaanza kuingia kidogokidoga.

Kuna sababu ninaweza kuitamka wazi, ni kwamba, na mimi nimepitia vipindi vigumu. kweli kuna mapambano katika safari yetu ya imani, na hata kama mtu hapendi kuyasimulia, yapo kabisa. 

Lakini mtu akiishiwa nguvu na kupoteza matumaini ataweza kumaliza vizuri safari yake ya imani, Mungu mwenyewe huwa anamwonekania, akimpa Neno lenye nguvu, la kumhuisha na kumwinua tena: 

Warumi 14:7,8  Kwa sababu hakuna mtu miongoni mwetu aishiye kwa nafsi yake, wala hakuna afaye kwa nafsi yake.  Kwa maana kama tukiishi, twaishi kwa Bwana, au kama tukifa, twafa kwa Bwana.  Basi kama tukiishi au kama tukifa, tu mali ya Bwana. 

Mtume Paulo aliyeandika maneno hayo, alipitia mapambano ya hatari sana. Na kwa uelewa wetu, hatimaye aliuawa kwa ajili ya kutangaza habari za Kristo aliyefufuka. Lakini mapema tu katika huduma yake, alifanya maamuzi kuweka msimamo kabisa.  Nikiishi au nikifa, mimi ni mali ya Bwana. 

Sasa dua ninayokuombea leo ni kwamba, Neno la Mungu liweze kutia ujasiri usioweza kutikisika ndani ya moyo wako.  Ukiishi au ukifa, uwe na msimamo.  Wewe ni mali ya Bwana. 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.


We use cookies to improve your browsing experience, analyse site traffic & personalise content, but we do not track you when you leave this site. To find out how we utilise & protect your data, check out our "Privacy Policy".

Privacy Policy