Uwezo Mkubwa wa Maneno
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Mithali 18:21 Mauti na uzima huwa katika uwezo wa ulimi; na wao waupendao watakula matunda yake.
Laiti tungeelewa uwezo mkubwa wa maneno yetu, ingekuwa vizuri sana Niliwahi kumsikia mtu mmoja akisema kwamba, maneno tunayowaambia watu wengine yanaweza kuleta uzima au mauti, na ni kweli kabisa.
Niliangalia video kwenye YouTube hivi karibuni, sasa ile video ilikuwa inahusu mada hii, Yule ndugu alikuwa anasimulia habari za rafiki yake wa karibu aliyejaribu kila wakati kutafuta kukubaliwa na baba yake. Lakini baba yake alikuwa msimamizi mkali sana na hakuweza kumpongeza wala kumtia moyo mwanae hata siku moja.
Sasa, rafiki yake alipokuwa chuo kikuu, alipata maksi nzuri sana, yaani A katika masomo yote. Kijana akawaza moyoni mwake kwamba Bila shaka, safari hii baba yangu atasema, “hongera mwanangu”. Bila shaka angepewa kibali alichokitamani sana kwa baba yake. Kwa hisia kali alimpigia simu baba yake na akaanza kumsimulia habari hiyo nzuri.
Jibu la baba yake? “Niko bizi sana sasa hivi, nitakupigia baadaye.” Na wala hakumpigia tena, yule kijana alikatishwa tamaa mno. Alianza kutumia dawa za kulevya na pombe na baada ya kipindi fulani alikufa kwa kuzidisha matumizi ya dawa hizo. Hapo ndipo mnenaji kwenye ile video alisisitiza yafuatayo: kinywa chako kinaweza kutoa sumu au kinaweza kuleta uponyaji kwa nafsi iliyoumia. Na hili ndilo lengo la Mungu mwenyewe alolitaka pale aliposisitiza kwenye mstari huu :
Mithali 18:21 Mauti na uzima huwa katika uwezo wa ulimi; na wao waupendao watakula matunda yake.
Je!, Ulimi wako unanena nini? Je!, Uko tayari kupokea matokeo ya maneno yako? Acha niseme tena, maneno yana uwezo wa kuleta mema na uwezo wa kuleta mabaya.
Mauti na uzima huwa katika uwezo wa ulimi; na wao waupendao watakula matunda yake.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.