... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Uwezo wa Kuhisi Maono ya Mwingine

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Mathayo 7:12 Basi yo yote myatakayo mtendewe na watu, nanyi watendeeni vivyo hivyo; maana hiyo ndiyo torati na manabii.

Listen to the radio broadcast of

Uwezo wa Kuhisi Maono ya Mwingine


Download audio file

Uwezo wa kuhisi maono ya mwingine unaonyesha upendo unaovutia tena wenye nguvu kuliko hisia zote za binadamu.  Kumjali mtu na kuumia pamoja naye, au kushangilia pamoja naye, kunaonyesha upendo mkuu kuliko tendo lo lote lingine.

Kweli, uwezo wa kuhisi maono ya mwingine ni jambo linalopendeza mno.  Lakini katika pirika pirika za maisha; mtu huwa anajitahidi kutimiza kazi zake na kupambana na changamoto zake na hisia zake mwenyewe, mara nyingi tunasahau kujali watu wengine.

Ebu jaribu kufikiria ilivyokuwa jana au juzi wakati ulipokuwa pamoja na watu wegnine. mlipokuwa mnaongea, au kukaa pamoja tu, au kufanya kazi pamoja … haijalishi mlikuwa wapi, je!  Uliwahi kujiuliza hawa wengine wanafikiri nini!…Ulihisi maono yao!…Uliwaonyesha kwamba umewaelewa mahali waliopo!?

Labda unafikiri kwamba ninataka kuvuka mpaka na kujiingiza katika hisia zako, wakati wewe unapambana na maisha ya kila siku.  Basi, acha nijaribu kutafsiri uwezo huo wa kuhisi wanavyohisi wengine katika zoezi linaloeleweka.  Yesu alisema hivi: 

Mathayo 7:12  Basi yo yote myatakayo mtendewe na watu, nanyi watendeeni vivyo hivyo; maana hiyo ndiyo torati na manabii.

Hilo ni agizo la Yesu kujaribu kuwaelewa na kuhisi wanavyohisi watu wengine; na kuwatendea kama vile unavyotaka kutendewa.  Ukitafakari kidogo, utaona kwamba hii ndio sababu  ya kuwa na uwezo wa kuhisi maono ya mtu mwingine.

Ni kujali mwingine kwa jinsi ya kumwonyesha wazi kwamba umemwelewa; kwamba kwa kweli unahisi anavyohisi yeye.

Yo yote myatakayo mtendewe na watu, nanyi watendeeni vivyo hivyo.  

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.


We use cookies to improve your browsing experience, analyse site traffic & personalise content, but we do not track you when you leave this site. To find out how we utilise & protect your data, check out our "Privacy Policy".

Privacy Policy