... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Uwiano Kati ya Hatari na Thawabu

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Mathayo 5:11,12 Heri ninyi watakapowashutumu na kuwaudhi na kuwanenea kila neno baya kwa uongo, kwa ajili yangu. Furahini, na kushangilia; kwa kuwa thawabu yenu ni kubwa mbinguni; kwa maana ndivyo walivyowaudhi manabii waliokuwa kabla yenu.

Listen to the radio broadcast of

Uwiano Kati ya Hatari na Thawabu


Download audio file

Kila mtu ana kiwango chake cha uwiano kati ya kuthubutu mambo na matazamio yake ya kujipatia thawabu katika maisha yake. Kuna wengine wanaweza kujaribu mambo makuu ili wapate thawabu nyingi, Wengine ni wataratibu, hawawezi kuthubu kufanya makuu bali wanajaribisha mambo kwa wastani wakiridhika kuendelea na maisha ya usalama.

Sasa, ukitafakari hayo, nwewe uko wapi katika uwiano huo? 

Kuna watu wanabahatisha kwa kuacha thawabu ndogo ambazo wangepata sasa hivi ili waweze kupata thawabu kubwa mbeleni.  Gazeti la the Wall Stree Journal, lilimnukuu daktari mtafiti aitwaye Kaileigh Byrne akisema: “Watu, mara nyingi wanapendelea kupokea tuzo mara moja, wakijiridhisha na mafao ya haraka kuliko kuvuta subira ili wapokee mafao ya baadaye yaliyo makubwa zaidi.”  Naona kama dakatari huyo amesema ukweli kabisa. 

Jaribu kutafakari, hivi, uko tayari gharama ya mahusiano yako na Yesu, uko tayari kukabiliana na na hatari iliyoko mbele yako ili upate thawabu kubwa kwa baadaye. 

Mathayo 5:11,12  Heri ninyi watakapowashutumu na kuwaudhi na kuwanenea kila neno baya kwa uongo, kwa ajili yangu.  Furahini, na kushangilia; kwa kuwa thawabu yenu ni kubwa mbinguni; kwa maana ndivyo walivyowaudhi manabii waliokuwa kabla yenu. 

Sasa, mwitikio wako uko wapi watu watakapokushutumu, watakapokuudhi na kukunenea mabaya kwasababu unamfuata Yesu?  Utashangaa au utaumia?  Au utataka kujilipiza kisasi?  Labda kujilipiza kisasi kungekuridhisha angalau kidogo kwa muda huo, au ungeweza kuvuta subira na kukubali kuahirisha thawabu yako. Ukipenda, Unaweza kufurahi na kushangilia.  Kwa nini?  Ni kwasababu kuna thawabu kubwa mno inayokusubiri huko mbinguni.  

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.


We use cookies to improve your browsing experience, analyse site traffic & personalise content, but we do not track you when you leave this site. To find out how we utilise & protect your data, check out our "Privacy Policy".

Privacy Policy