... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Visivyoweza Kutetemeshwa

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Waebrania 12:27-29 Lakini neno lile, Mara moja tena, ladhihirisha kuhamishwa vile viwezavyo kutetemeshwa, kama vitu vilivyoumbwa, vitu visivyoweza kutetemeshwa vikae. Basi kwa kuwa tunapokea ufalme usioweza kutetemeshwa, na mwe na neema, ambayo kwa hiyo tumtolee Mungu ibada ya kumpendeza, pamoja na kicho; maana Mungu wetu ni moto ulao.

Listen to the radio broadcast of

Visivyoweza Kutetemeshwa


Download audio file

Ukatili wa dunia hii dhidi ya imani ya Wakristo umeendelea tangu miaka elfu mbili.  Lakini siku hizi uvamizi huo umefikia msisimko mkubwa sana, Wakristo wengi wakiuawa katika miaka 100 iliyopita kuliko katika karne zote 19 kabla ya hapo.

Hoja za watu wa ulimwengu huu dhidi ya imani ya Kikristo zina nguvu.  Ikiwa kwenye eneo la mapambano yanayohusu jinsia, au hoja shupavu za wakana Mungu wakivizia kanisa lisilokamilika kabisa, kumbe sio rahisi kuwa Mkristo mnyenyekevu anayeamini Biblia katika karne yetu ya 21.  Sijui kama umeshagundua hayo?

Lakini tutulie kwanza na kujaribu kurekebisha mtazamo wetu: 

Waebrania 12:27-29  Lakini neno lile, Mara moja tena, ladhihirisha kuhamishwa vile viwezavyo kutetemeshwa, kama vitu vilivyoumbwa, vitu visivyoweza kutetemeshwa vikae.  Basi kwa kuwa tunapokea ufalme usioweza kutetemeshwa, na mwe na neema, ambayo kwa hiyo tumtolee Mungu ibada ya kumpendeza, pamoja na kicho; maana Mungu wetu ni moto ulao. 

Ngome zote zilizosimamishwa kinyume cha ufalme wa Mungu, hoja zote zinazouvizia, siku moja zitaangamizwa.  Hata vilivyoumbwa vyote vitateketea na kitakachobaki ni ufalme wa Mungu usioweza kutetemeshwa kamwe. 

Kwa hiyo, katikati ya mapambano hayo (ambayo Kristo tayari ameshashinda) kazi yako na kazi yangu, si kufadhaika wala kuhofu tukivamiwa, wala kupoteza tumaini letu – bali ni kumwabudu Mungu, kumheshimu na kumwogopa yeye. 

Kwa hiyo, jipe moyo.  Ufalme wa Mungu hauwezi kutetemeshwa.  Jipe moyo. 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.


We use cookies to improve your browsing experience, analyse site traffic & personalise content, but we do not track you when you leave this site. To find out how we utilise & protect your data, check out our "Privacy Policy".

Privacy Policy