Wakati Rafiki Wanakukimbia
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Mithali 19:4 Utajiri huongeza rafiki wengi; bali maskini hutengwa na rafiki zake.
Hakuna jambo ambalo linashtua mtu na kumwangusha na kumwumiza kama rafiki anayekuwa karibu naye vipindi vizuri lakini kipindi kigumu anamkimbia. Sijui kama wewe umeshaona hayo?
Haipendezi kabisa. Wakati mambo yako vizuri sana, watu wote wanataka kuwa rafiki yako. Wakati unaharibikiwa, wakati hisia zako zinavurugika na maisha yako inachafuliwa, baadhi ya wanaojiita rafiki zako watarudi nyuma na kujitenga na wewe.
Si jambo jipya hata kidogo. Zaidi ya miaka elfu tatu iliyopita, Mfalme mwenye hekima aitwaye Sulemani alieleza hivi:
Mithali 19:4 Utajiri huongeza rafiki wengi; bali maskini hutengwa na rafiki zake.
Inabidi sasa kila mmoja wetu ajiulize, je! Mimi ni rafiki aina gani? Mimi ni rafiki kipindi kizuri tu, kama vile mmojawapo wa wale wanaopenda kuwa karibu ya watu waliofanikisha mambo yao, lakini najitenga na watu wenye shida? Au mimi ni rafiki kweli anayekuwa karibu katika hali zote?
Kwa hiyo, acha nikuulize moja kwa moja. Je! Wewe ni rafiki aina gani? Ebu fikiria habari ya watu unaojuana nao – wanaostawi na wanaofisirika. Je! Unawafanyia ubaguzi? Je! Unavutwa zaidi kwa wanaostawi na kujitenga na wenye shida?
Ni kweli, huu ni mtazamo wa kawaida kwa sababu kila mtu anataka kutegemezwa. Lakini pia, sote tunahitaji kuwa na mahusiano pale ambapo ni sisi wenyewe tuna la kutoa na kusaidia, sio kupokea tu.
Utajiri huongeza rafiki wengi; bali maskini hutengwa na rafiki zake. Usiwe mtu anayetupa rafiki yake wakati wa shida.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.