Walakini … Pendo
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Zaburi 73:21-24 Moyo wangu ulipoona uchungu, viuno vyangu viliponichoma, nalikuwa kama mjinga, sijui neno; nalikuwa kama myama tu mbele zako. Walakini mimi ni pamoja nawe daima, umenishika mkono wa kuume. Utaniongoza kwa shauri lako, na baadaye utanikaribisha kwa utukufu.
Bila shaka, pendo la mtu kwetu linakuwa bora wakati hatustahili; wakati anachukuliana nasi wakati tuna uchungu moyoni, wakati tunatenda kwa ujinga na ukatili. Hicho ndicho kilele cha upendo.
Sisi sote tumewahi kuwa na uchungu moyoni. Sisi sote tumewahi kutenda visivyo. Sisi sote tumepitia hali kama hiyo. Kama uliweza kufuata kipindi cha jana, utakumbuka nilivyosema kwamba uchungu moyoni kuhusu mabaya yaliyotupata na matendo yasiyofaa yanayofuata haina faida yo yote kwetu au kwa mwingine.
Na kweli, haina faida hata kidogo. Lakini kujikwamua kutoka hali hiyo siyo rahisi. Kuna wakati hatuwezi kabisa. Kinachohitajika ni mtu kukupenda licha ya hali yako wakati hustahili labda. Mtu aliye tayari kuchukuliana na wewe wakati bado unatenda kwa ukatili.
Tumsikilize tena mtunga zaburi, akielekeza dua lake kwa Mungu:
Zaburi 73:21-24 Moyo wangu ulipoona uchungu, viuno vyangu viliponichoma, nalikuwa kama mjinga, sijui neno; nalikuwa kama myama tu mbele zako. Walakini mimi ni pamoja nawe daima, umenishika mkono wa kuume. Utaniongoza kwa shauri lako, na baadaye utanikaribisha kwa utukufu.
Jamaa huyu alikuwa na uchungu akimtendea Mungu kwa ujinga na ukatili. Ni orodha inayotisha kabisa. Hata hivi … Mungu hakumwacha, bali alimshika na mkono wake wa kuume, na kumshauri na baada ya kumwongoza kupitia yote, Mungu alimkaribisha kwake katika utukufu.
Na hii, ni kilele kabisa cha upendo, upendo ule ule Mungu anao kwako kipindi chako chenye giza nene. Kamwe hatakuacha au kukutupa. Atakuongoza kupitia yote hadi akufikishe ndani ya utukufu wake.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.