Wanaokutendea Jeuri.
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Mithali 12:16 Ghadhabu ya mpumbavu hujulika mara; bali mtu mwerevu husitiri aibu.
Mimi ninaona kwamba karibu kila siku, ninakutana na watu ambao wanajaribu kunitukana na kunikwaza kwa njia tofauti tofauti. Je! Umeshakutana na hayo?
Watu wengi ingawa sio wote katika pande zote za siasa ulimwenguni wamekuwa hawapendani tena , bali wamekuwa mabingwa wa kutukanana … hali inayotaka kuleta mpasuko katika jamii.
Lakini si katika siasa tu, bali katika sekta mbalimbali pia… Na ikiwa uko kama mimi, hali hiyo inafadhaisha na inachukiza kwa kweli.
Kwa hiyo … acha nikuonyeshe hekima ya kimungu inayoweza kukusaidia kukabiliana na hali hiyo:
Mithali 12:16 Ghadhabu ya mpumbavu hujulika mara; bali mtu mwerevu husitiri aibu.
Yaani, mtu akitendewa vibaya, hapo hapo anataka kurudisha tusi, kujibu vikali kwa ajili ya kulinda heshima yake.
Lakini Mungu anasema kwamba kughadhibika kwa haraka ni upumbavu. Bali mwenye hekima anajizuia asirudishe matusi. Au, kama vile mtu mwingine alivyosema …
“Tunao uwezo wa kukataa kukwazika. Wakati watu wanakupuuza au kama wanakuumiza makusudi … kwa kweli wanajionyesha walivyo wao wenyewe. Wanadhihirisha yaliyomo ndani yao, si yaliyomo ndani yako. Sasa jinsi unavyowatendea wanaokutendea vibaya, inaonyesha kiwango cha kukomaa kwako kihisia na kiroho.”
Ghadhabu ya mpumbavu hujulika mara; bali mtu mwerevu husitiri aibu.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.