Watawala Wakipoteza Mamlaka Yao
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
1 Wakorintho 2:6 Walakini iko hekima tusemayo kati ya wakamilifu; ila si hekima ya dunia hii, wala ya hao wanaoitawala dunia hii, wanaobatilika.
Mtu akichunguza mazingira ya ulimwengu huu, ataona kwamba kuna madikteta wanaotawala nchi baadhi, wanaoamuru watu jinsi wanavyopaswa kuishi hata yale ambayo wanayotakiwa waamini. Haipendezi kweli.
Lakini utawala kama huo wenye mamlaka yote kumbe! Yanaweza kuwa yametukaribia zaidi ya jinsi tunavyofikiria. Hata kama unaishi katika uhuru kiasi kama vile mimi, zaidi na zaidi tunaambiwa ni yapi yatupasa kuyawaza na kuyaamini … na ole kwake yule atakayepaza sauti kuyapinga.
Katika nchi yangu mimi, nchi inayo demokrasia halisi, kuna mambo mengine ambayo ninayaamini na moyo wangu wote, lakini siwezi kuyatamka hewani kwa hofu kwamba kituo cha redio kingeweza kufutiwa leseni yake.
Hailishi unaishi chini ya serikali gani, tena ukumbuke kwamba ujumbe huu wetu utatangazwa kote ulimwenguni siku hii ya leo … kadiri umma unavyoenda mbali na upendo wa Mungu, ndipo sisi wenyewe tutapelekwa mbali na upendo wa Mungu, pia ndipo inatajwa kuwa hekima ya sisi binadamu itazidi kupotoshwa.
Lakini hilo si jambo jipya hata kidogo. Sikiliza alivyoandika Mtume Paulo kuhusu mada hiyo hiyo takriban miaka 2,000 iliyopita.
1 Wakorintho 2:6 Walakini iko hekima tusemayo kati ya wakamilifu; ila si hekima ya dunia hii, wala ya hao wanaoitawala dunia hii, wanaobatilika.
Rafiki yangu, muda huu huu tunavyoongea, mamlaka ya wale ambao wanaotaka kutawala mawazo yetu na imani yetu, yanaanza kubatilika. Usiogope kuruhusu hekima ya Mungu – hekima isiyo ya ulimwengu huu – kujaza moyo wako … ili uweze kuishi katika ushindi wa upendo wake.
Na Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.