Waza Juu ya Mambo ya Mungu
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Mathayo 16:21-23 Tangu wakati huo Yesu alianza kuwaonya wanafunzi wake ya kwamba imempasa kwenda Yerusalemu, na kupata mateso mengi kwa wazee na wakuu wa makuhani, na waandishi, na kuuawa, na siku ya tatu kufufuka. Petro akamchukua, akaanza kumkemea, akisema, Hasha, Bwana, hayo hayatakupata. Akageuka, akamwambia Petro, Nenda nyuma yangu, Shetani; u kikwazo kwangu; maana huyawazi yaliyo ya Mungu, bali ya wanadamu.
Kuna mvutano mkubwa kati ya mambo ya ulimwengu huu na hekima ya Mungu inayoonekana kuwa kinyume cha mantiki ya binadamu.
Najiuliza, je! Umewahi kusikia mvutano huo moyoni mwako. Natumaini kwamba umeusikia kwa sababu dunia hii inawavuta binadamu kufuata barabara ile pana na rahisi inayopeleka watu kwenye uharibifu. Lakini Yesu anawaita watu wengine kupita kwenye mlango mwembamba na kufuata njia ngumu iendayo uzimani.
Ndiyo maana kuna mvutano ndani ya kila mtu anayekusudia kuwa mwanafunzi wake. Mantiki ya kibinadamu inatwambia kwamba lazima maisha yawe rahisi, lazima tupate mafanikio, lazima tupate yale ambayo tunayatamani. Lakini hekima ya Mungu inasimama kinyume kabisa na mantiki ile ya ubinafsi.
Mathayo 16:21-23 Tangu wakati huo Yesu alianza kuwaonya wanafunzi wake ya kwamba imempasa kwenda Yerusalemu, na kupata mateso mengi kwa wazee na wakuu wa makuhani, na waandishi, na kuuawa, na siku ya tatu kufufuka. Petro akamchukua, akaanza kumkemea, akisema, Hasha, Bwana, hayo hayatakupata. Akageuka, akamwambia Petro, Nenda nyuma yangu, Shetani; u kikwazo kwangu; maana huyawazi yaliyo ya Mungu, bali ya wanadamu.
Unaona. Petro alikuwa anatumia mantiki ya kibinadamu ambayo tungetumia mimi na wewe kwa silika ya asili. Alitaka kumweka sawa Yesu, atumie busara. Alitaka kumlinda jamani! Lakini alilolifanya Petro lilileta mwitikio mkali sana kuliko karipio lo lote tunalosoma katika Maandiko. Je! Ungejisikiaje kama Yesu angekujibu hivyo?
Hata ikitisha sana, bora uweke mawazo yako juu ya mambo ya Mungu!
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.