Wema na Maarifa
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
2 Petro 1:3,5 Kwa kuwa uweza wake wa Uungu umetukirimia vitu vyote vipasavyo uzima na utauwa, kwa kumjua yeye aliyetuita kwa utukufu wake na wema wake mwenyewe ... Naam, na kwa sababu iyo hiyo mkijitahidi sana kwa upande wenu, katika imani yenu tieni na wema, na katika wema wenu maarifa.
Wengi wetu tunataka kutenda mema. Tunataka kuwa wastaarabu na wenye huruma. Tunataka kufanya maamuzi yaliyo sahihi. Lakini wakati mtu anaamka asubuhi, mara ingine mambo hayaendi kama alivyokusudia. Kwa nini?
Swala la kunia kutenda mema na kuishi kama inavyotakiwa ni jema … ili kutekeleza ni gumu, hususani pale mtu hajui jinsi ya kufanya. Kama mtu anataka kuwa rubani wa kuongoza ndege, lazima ajifunze na kusomea fani hiyo, si kweli? Sasa kuishi maisha vizuri nakwambia, ni vigumu kuliko kuendesha ndege angani.
Kwa hiyo, kama tunataka kubadilisha mwenendo unayotuharibia maisha bora tunaYotamani kuishi – yaani tabia zetu mbaya kama vile kufokea watu au kuwapuuza na kadhalika – lazima tujue la kufanya.
Tayari Mungu ameshatukirimia uwezo na vipaji na karama vinavyohitajika kwa kuishi maisha yale tunayotamani. Kwa hiyo ni muda mwafaka kushirikiana naye kwa kufikia lengo:
2 Petro 1:3,5 Kwa kuwa uweza wake wa Uungu umetukirimia vitu vyote vipasavyo uzima na utauwa, kwa kumjua yeye aliyetuita kwa utukufu wake na wema wake mwenyewe … Naam, na kwa sababu iyo hiyo mkijitahidi sana kwa upande wenu, katika imani yenu tieni na wema, na katika wema wenu maarifa.
Leo tunataka kuangalia vizuri habari ya wema na maarifa. Rafiki yangu, ujue kwamba Neno la Mungu limejaa hekima yake. Hekima inayotufafanulia mambo mengi, pia hekima ya Roho Mtakatifu inayotuwezesha kwa uweza wake – ili tubadilike. Kwa hiyo kwa imani yako tia wema na maarifa pia.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.