Wewe ni Mtoto wa Nani?
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
1 Yohana 3:9,10 Kila mtu aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi, kwa sababu uzao wake wakaa ndani yake; wala hawezi kutenda dhambi kwa sababu amezaliwa kutokana na Mungu. Katika hili watoto wa Mungu ni dhairi, na watoto wa ibilisi nao. Mtu ye yote asiyetenda haki hatokani na Mungu, wala yeye asiyempenda ndugu yake.
Mwenendo wako, jinsi unavyowatendea wengine vinadhihirisha kabisa jinsi wewe ulivyo na yale ambayo unayoyaamini. Kwa hiyo niulize, je! Unaenendaje? Unawatendeaje watu wengine?
Ninachokijuta zaidi ni kwamba sikuwasikiliza vizuri wazazi wangu wakati nilikuwa kijana wala sikujifunza kutokana na hekima yao wala kuishi mapema sawa sawa na busara zao. Matokeo ni kwamba nilifanya makosa mengi na nimekula hasara.
Kwa hiyo, kinachoniamsha nitoke kitandani alfajiri karibia kila asubuhi na kuandaa vipindi hivi vya NENO SAFI LENYA AFYA kwa ajili yako na kwa ajili ya wengine wengi, ni kukusaidia ujiepushe na makosa niliyoyatenda mimi
1 Yohana 3:9,10 Kila mtu aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi, kwa sababu uzao wake wakaa ndani yake; wala hawezi kutenda dhambi kwa sababu amezaliwa kutokana na Mungu. Katika hili watoto wa Mungu ni dhairi, na watoto wa ibilisi nao. Mtu ye yote asiyetenda haki hatokani na Mungu, wala yeye asiyempenda ndugu yake.
Rafiki yangu, ninakusihi leo, msikilize Baba yako wa Mbinguni. Umwendee yeye Mungu halafu bega kwa bega mkabiliane na dhambi maishani mwako moja kwa moja kwa kukata shauri kabisa. Uishi kwa neema yake na uwezo wake kama mtoto wake si kama mtoto wa Shetani.
Kwa sababu jinsi unavyoishi, yaani mwenendo wako, unadhihirisha kama wewe ni mtoto wa nani.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.