... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Wosia wa Baba kwa Mwanaye

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

1 Nyakati 28:9 Nawe, Sulemaini mwanangu, mjue Mungu wa baba yako, ukamtumikie kwa moyo mkamilifu, na kwa nia ya kumkubali; kwa kuwa BWANA hutafuta-tafuta mioyo yote, na kuyatambua mawazo yote ya fikira; ukimtafuta, ataonekana nawe; ukimwacha, atakutupa milele.

Listen to the radio broadcast of

Wosia wa Baba kwa Mwanaye


Download audio file

Mahusiano ya kipekee tunayoweza kuwa nayo maishani ni kuwa mzazi.  Lakini hata kama wewe si mzazi, bado unaweza kufikiria namna mahusiano ya kipekee.

Sisi kama wazazi tunawatakia watoto wetu mambo bora.  Kwa hiyo, ukiwa kam mzazi au hata kama hujawa na watoto, Ungependa kumrithisha mtoto wako hekima gani?, Ni ushauri gani ungewapa watoto wako hata baada yaw ewe kuondoka? 

Katika uzee wake Mfalme Daudi alimrithisha mwanae Sulemani maneno ya hekima yenye thamani sana. 

1 Nyakati 28:9  Nawe, Sulemaini mwanangu, mjue Mungu wa baba yako, ukamtumikie kwa moyo mkamilifu, na kwa nia ya kumkubali; kwa kuwa BWANA hutafuta-tafuta mioyo yote, na kuyatambua mawazo yote ya fikira; ukimtafuta, ataonekana nawe; ukimwacha, atakutupa milele. 

Ni maneno sahili lakini yenye nguvu.  Kwa moyo wako wote na nguvu zako zote, umjue Mungu na kumtumikia. Pia mtumikie kwa moyo safi, moyo mweupe, moyo wa shukrani.  Kwa sababu ukiwa umejiandaa hivyo, atakuona na utakuwa na kibali kumwendea muda wowote upate msaada. 

Ni jambo jema kabisa kuwa na kibali na kumwendea Mungu na kupata msaada na majibu unayohitaji …  moyo wako unapokuwa safi kwa kumwelekea na hata kuonekana kuwa na moyo mweupe kwa wale wanaokuzunguka ukiwa na mtazamo sahihi. 

Rafiki yangu, haijalishi uko wapi muda huu, haijalishi unapambana na nini, fuata ushauri wa Sulemani. Ruhusu Roho Mtakatifu kulainisha moyo wako leo katikati ya mazingira uliyomo. 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.


We use cookies to improve your browsing experience, analyse site traffic & personalise content, but we do not track you when you leave this site. To find out how we utilise & protect your data, check out our "Privacy Policy".

Privacy Policy