Yabadilishe Mashaka Yawe Matazamio
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Zaburi 18:3-6 Nitamwita BWANA astahiliye kusifiwa, hivyo nitaokoka na adui zangu. Kamba za mauti zilinizunguka, mafuriko ya uovu yakanitia hofu. Kamba za kuzimu zilinizunguka, mitego ya mauti ikanikabili. Katika shida yangu nalimwita BWANA, na kumlalamikia Mungu wangu. Akaisiki sauti yangu hekaluni mwake.
Niruhusu leo niongee habari ya neno hili: mashaka. Mara moja neno lile linapeleka mawazo kwenye hofu na kukosa amani, mtu akifikiri yatakayoweza kumjia.
Hakuna mtu angependa kwa hiari yake kuishi daima katika hali ya mashaka, au sio? kadiri tunavyoendela kuishi katika ulimwengu huu, kuna vitisho, hatari na wasiwasi ambavyo vinaweza kutupelekea kuwa na mashaka-mashaka.
Hata kama woga ni mwitikio wa asili ya mwanadamu kulinda usalama wake, kwa mtu aliyeweka imani yake kwake Yesu, hisia ile ya mashaka ni hali ambayo inambidi aishinde, tena anaweza kuishinda.
Umsikilize Mfalme Daudi aliyepitia vitisho miaka mingi na kuhofia uhai wake, halafu utafakari.
Zaburi 18:3-6 Nitamwita BWANA astahiliye kusifiwa, hivyo nitaokoka na adui zangu. Kamba za mauti zilinizunguka, mafuriko ya uovu yakanitia hofu. Kamba za kuzimu zilinizunguka, mitego ya mauti ikanikabili. Katika shida yangu nalimwita BWANA, na kumlalamikia Mungu wangu. Akaisikia sauti yangu hekaluni mwake.
Daudi kamwe hakusita kudhihirisha hofu zake. Kwa kweli alitishiwa vikali kabisa. Lakini wakati alizimwaga mbele zake Mungu … utaona jinsi mara tena na tena mashaka yake yakageuka kuwa matazamio mema.
Kadiri alivyotoa macho yake kwenye vitisho vilivyomkabili na kuyainua juu kwa Mungu, ndipo moyo wake ulithibitika. Ndipo alianza kutazamia atakavyotenda Mungu. Hii inatokea wakati mtu anaomba. Mashaka yanageuka kuwa matazamio.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.