Acha Uzima Uanze
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
1 Petro 1:3 Ahimidiwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, ambaye kwa rehema zake nyingi alituzaa mara ya pili ili tupate tumani lenye uzima kwa kufufuka kwake Yesu Kristo katika wafu.
Kristo amefufuka! Amefufuka kweli kweli! Ni kiitikio cha zamani cha Wakristo kupitia makarne mengi. Ni kelele za shangwe. Lakini, je! Ina maana yo yote kwetu baada ya miaka elfu mbili?
Vipi? Kufufuka kwake Yesu Kristo kuna maana gani kwako, au hakuna maana yo yote, leo hii, mahali ulipo katika pirika za maisha, baada ya muda mrefu tangu Yesu alitangaziwa kwamba amefufuka kutoka wafu?
Au leo, utafanya tu kama wengi wanavyofanya wakiandaa mchezo ya watoto wakitafuta mayai na chokoleti izidiyo, baadaye kula na kushiba na kwenda kulala, basi?
Miaka isiyo michache baada ya Jumapili ile ya Pasaka, Mtume Petro – kumbuka kwamba yeye ndiye aliyemkana Yesu mara tatu usiku ule kuamkia siku aliyosulubiwa – aliwaandika Wakristo waliokuwa wanateswa vibaya maneno yafutatayo:
1 Petro 1:3 Ahimidiwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, ambaye kwa rehema zake nyingi alituzaa mara ya pili ili tupate tumani lenye uzima kwa kufufuka kwake Yesu Kristo katika wafu.
Waliotangulia kusoma maneno hayo inawezekana kwamba walikuwa wanajiuliza ni lini Warumi watakuja kuwatesa vikali na kuwapaka lami ili wawatumie kama mienge ya kuangaza usiku sherehe ya mfalme wa wafalme.
Lakini Petro, hapo hapo anawaangazia habari ya maisha mapya. Uzima kamilifu, mpya. Si kwa kutumia lugha ya mashaka, “Natumaini kesho sitateswa,” hapana. Ni tumaini lenye uzima kwa kufufuka kwake Yesu Kristo katika wafu.
Haijalishi kikutokee nini, tumaini lile haliwezi kufa kwa sababu Yesu alifufuka kutoka kaburi. Kristo amefufuka. Amefufuka kweli kweli!
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.