Ahadi za Mungu Ambazo Hazijatimia
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Waebrania 11:13 Hawa wote wakafa katika imani, wasijazipokea zile ahadi, bali wakaziona tokea mbali na kuzishangilia, na kukiri kwamba walikuwa wageni, na wasafiri juu ya nchi.
Acha nikuibie siri, Mimi ninatamani Mungu anibariki. Ameahidi mengi kwenye Biblia, ninataka anitimizie ahadi zote –tena ikiwezekana leo hii, au isipite wiki hii– pia azifungie pamoja ndani ya catoni iliopambwa vizuriii. Sijui wewe?
Ndio matazamio yetu, sindiyo? Tunajua kwamba haiwezikani, tena haieleweki, lakini bado tunasema hivi … “Kwa kuwa Mungu ni Mungu wa baraka, basi natamani kupata baraka zote ziwezekanavyo tena sasa hivi!” Dhana kama hiyo inatokana na mtazamo wa kisasa uliojengwa juu ya ubinafsi na mfumo wa kujaribu kujikusanyia mali tu.
Nipate simu janja ya gharama kubwa, Nikatalii kwenye nchi za mbali na kukaa kwenye hoteli za kifahari. Nguo, magari … cho chote kile kinachokupendeza kwa dakika hii. Tunavutwa na kushawishika na matangazo yanayosisimka. “Kwa nini mimi nisipate kushiriki na kufurahia mambo hayo kama wanavyofanya wengine?!”
Hatuwezi kuacha kutaja ahadi za Mungu – Yeye ni Mungu aponyaye… lakini bado watu wake wanaugua na wanakufa. Tunatamani kupata yale tunayotaka, tunataka Mungu awajibike na kutupa yote tunayotamani na ikitokea hatimizi matarajio yetu hapo huwa tunaona kama ametuangusha japokuwa tunafahamu kwamba mtazamo huo ni potovu kabisa.
Katika kitabu cha Waebrania kinachopatikana kwenye Agano Jipya, katika sura ya 11 habari za mashujaa, wanawake kwa wanaume, mashujaa wa imani – akina Abeli, Henoko, Nuhu, Ibrahimu, Sara n.k. … lakini maandiko yanaendelea kwakusema hivi:
Waebrania 11:13 Hawa wote wakafa katika imani, wasijazipokea zile ahadi, bali wakaziona tokea mbali na kuzishangilia, na kukiri kwamba walikuwa wageni, na wasafiri juu ya nchi.
Kumbukumbu: Ni kweli, Mungu anataka kunibariki, lakini sidhani kama atanitimizia yote mara moja, sidhani.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.