... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Bado Anatafuta Wanafunzi

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Mathayo 4:21,22 Akaendelea mbele, akaona ndugu wengine wawili, Yakobo wa Zebedayo, na Yohana nduguye, ambao walikuwamo chomboni pamoja na Zebedayo baba yao, wakizitengeneza nyavu zao; akawaita. Mara wakakiacha chombo na baba yao, wakamfuata.

Listen to the radio broadcast of

Bado Anatafuta Wanafunzi


Download audio file

Unatazamia kuwa na mwaka wa namna gani katika mwaka huu mpya?  Yatakuwa yale yale tu au unatazamia matukio yasiyo ya kawaida?  Je!  Mwaka huu mpya utakuwaje kwako?

Kwa sehemu kubwa, wewe na mimi, hatuwezi kujua kilicho mbele.  Lakini tukianza mwaka huu mpya, kuna kitu kimoja ambacho tunaweza kukifanya ili maisha yetu angalau yasisimke.  Kinahusiana na matazamio yetu kwamba kumfuata Yesu kutatupeleka sehemu isiyo yakawaida. 

Jana tuliangalia namna ambavyo Yesu aliwaita Simoni Petro na nduguye Anderea wamfuate, na kweli walimfuata.  Lakini alikuwa bado anawatafuta wafuasi wengine. 

Mathayo 4:21,22  Akaendelea mbele, akaona ndugu wengine wawili, Yakobo wa Zebedayo, na Yohana nduguye, ambao walikuwamo chomboni pamoja na Zebedayo baba yao, wakizitengeneza nyavu zao; akawaita.  Mara wakakiacha chombo na baba yao, wakamfuata. 

Ebu fikiria yaliyotokea. Yesu alikuwa anawaita watu hawa, Yakobo na Yohana kwenye maisha ya wasiwasi.  Wao walikuwa wamezoa kuvua, usiku baada ya usiku mwingine, wakiwa na baba yao Zebedayo. Kupanda gezini, kushusha nyavu, kuvua, kurudi, kutengeneza vifaa, kuuza mapato sokoni.  Ilikuwa kazi yao ya kawaida waliyoizoea, lakini wakati Yesu anawaita wamfuate, mara wakakiacha chombo na baba yao, wakamfuata.  

Kumbe, bado Yesu anatafuta wanafunzi wa kumfuata.  Je!  Uko tayari?  Je unakubali kuondoka? 

Mara wakakiacha chombo na baba yao, wakamfuata.  

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.


We use cookies to improve your browsing experience, analyse site traffic & personalise content, but we do not track you when you leave this site. To find out how we utilise & protect your data, check out our "Privacy Policy".

Privacy Policy