... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Bahili au Mkarimu?

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Kumbukumbu 15:7,8 Kama akiwapo mtu maskini pamoja nawe, nduguzo mmojawapo, ndani ya malango yako mojawapo, katika nchi yako akupayo BWANA, Mungu wako, usifanye moyo wako kuwa mgumu, wala usimfumbie mkono wako nduguyo maskini; lakini mfumbulie mkono wako kwa kweli, umkopeshe kwa kweli yatoshayo haja yake katika ahitajiayo.

Wengi wetu hatujioni kuwa matajiri.  Inategemeana na mazingira yako, lakini inawezekana unajiona kuwa mtu wa kawadia, sio maskini lakini pia … si tajiri.  Lakini unapopita barabarani na kuona mzee akiombaomba unajisikiaje?

Mimi naona si haki kabisa kwamba mtu kutokana na mahali alipozaliwa na familia yake na mazingira ameyokulia hatimaye anakuwa tajiri au maskini.  Kwanini hayo?  Kwanini Mungu hashughulikii hapo? 

Amepashughulikia tayari, Maandiko yafuatayo yanalenga hasa sisi tunaojiona watu wa kawaida, “tabaka ya kati” tuseme – yaani, mimi niko sawa tu lakini si tajiri hata kidogo.

Kumbukumbu 15:7,8  Kama akiwapo mtu maskini pamoja nawe, nduguzo mmojawapo, ndani ya malango yako mojawapo, katika nchi yako akupayo BWANA, Mungu wako, usifanye moyo wako kuwa mgumu, wala usimfumbie mkono wako nduguyo maskini; lakini mfumbulie mkono wako kwa kweli, umkopeshe kwa kweli yatoshayo haja yake katika ahitajiayo. 

Ni ajabu vile mtazamo wetu sisi tunaoishi kwenye starehe za tabaka ya kati, namna unavyoweza kupotoshwa na hali zetu. Ukitaka kujua ukweli, kama unaweza kupata maji safi na chakula cha kutosha, nyumba na mavazi ya kutosha, kumbe wewe ni tajiri mno hata kama hujioni. 

Kwa hiyo tuulize, je! Matayari Mungu amewashughulikiaje?  Jibu ni kwamba:  Ametuagiza, wewe na mimi kuwa tayari kuwasaidia kwa moyo wa ukarimu watu maskini. 

Ndiyo, watu wanakuwa maskini kwa sababu mbalimbali.  Si kazi yetu kuhukumu.  Pia Mungu hataki tuishi tu kwa starehe na ubinafsi.  Bali alisema,  Usimfumbie mkono wako nduguyo maskini.  

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.