... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Ndani ya Meli ya Titanic

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Mariko 16:15,16 Akawaambia, Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe. Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini, atahukumiwa.

Listen to the radio broadcast of

Ndani ya Meli ya Titanic


Download audio file

Labda umeshasikia habari za meli iitwayo Titanic. Wakati inatengenezwa  zamani na kuingizwa majini tarehe 10 mwezi Aprili, 1912 watu walidai kwamba haiwezi kuzama; tena ilikuwa meli kubwa kuliko zote zilizokuwepo enzi hizo. Lakini siku tano tu baada ya kuanza safari yake ya kwanza kabisa, meli ile iligonga barafu baharini na ikazama.

Kati ya hesabu ya watu 2,224 abiria na mabaharia, zaidi ya watu 1,500 walikufa na tukio lile lilikuwa la maafa makubwa katika historia ya usafiri wa maji.  Kulikuwa na watu tabaka zote waliopanda meli ile kwa safari ile ya kwanza – matajiri, watu mashuhuri, wasomi – hawa kwenye daraja ya kwanza; hadi wasiosoma na maskini walikuwa daraja ya tatu pale chini. 

Lakini baada ya kugonga barafu ngumu na kuzama, walibandika tangazo kwenye ofisi ya shirikia lile la meli, kwenye tangazo lile waliandika tabaka mbili tu za watu – waliopotea na waliookolewa, basi.

Sasa leo hii ulimwenguni kwetu, kuna baa kubwa zaidi.  Haijalishi una utajiri kiasi gani kwa kufanikisha mambo yako au wewe ni mtu wa kawaida tu au maskini, ukweli ni kwamba, bado kuna tabaka mbili za watu:  waliopotea na waliookolewa. 

Mariko 16:15,16  Akawaambia, Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe.  Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini, atahukumiwa. 

Hayo ni maneno ya Yesu mwenyewe.  Na kuna sababu nakwambia ujumbe huu leo.  Yesu aliagiza wanafunzi wake kuenenda ulimwenguni mwote na kutangazia watu wote Habari yake Njema, ukiwemo wewe na mimi. 

Umwamini Yesu.  Umkabithi maisha yako yote mikononi mwake. Kama umeenda mbali naye, rudi.  Kwasababu ni kweli – kuna tabaka mbili za watu:  waliopotea na waliookolewa.  Anataka uokoke.  Yesu.  Umwamini. 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.