... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Ni Nani Atakayekwenda Mlangoni Kuangalia ni nani Anayebisha Hodi?

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Wakolosai 2:13-15 Na ninyi mlipokuwa mmekufa kwa sababu ya makosa yenu na kutokutahiriwa kwa mwili wenu, aliwafanya hai pamoja naye, akiisha kutusamehe makosa yote; akiisha kuifuta ile hati iliyoandikwa ya kutushitaki kwa hukumu zake, iliyokuwa na uadui kwetu; akaiondoa isiwepo tena, akaigongomea msalabani; akiisha kuzivua enzi na mamlaka, na kuzifanya kuwa mkogo kwa ujasiri, akizishangilia katika msalaba huo.

Listen to the radio broadcast of

Ni Nani Atakayekwenda Mlangoni Kuangalia ni nani Anayebisha Hodi?

Download audio file

Kuna siku nguvu za Shetani zinazokushawishi kwenda njia isiyofaa zinakuwa kama kubwa kuliko uwezo wako wa kumpinga hata kuliko uwezo wa Mungu kumzuia. Ndivyo inavyokuwa.

Mvutano huo mkubwa sisi sote tulio amua kumfuata Yesu tunaupitia – lakini kama hujaamua kumfuata Yesu, basi hakutakuwa na mvutano kwasababu njia ya shetani ni rahisi na itaonekana kwako kama jambo jepesi kulifanya. 

Lakini turejee kwa mtu anayeishi kwa unyenyekevu maisha ya imani ndanyi ya Yesu aliyekufa ili dhambi zake zipate kusamehewa, tena alifufuka ili aenende katika upya wa uzima. Kama wewe ni mtu yule utaelewa vizuri habari za mapambano na mivutano ninayoisema. 

Sasa acha nikuonyeshe mambo muhimu kutoka kwenye neno la Mungu kuhusu mambo muhimu yakupasayo kujua wakati wa jaribu: 

Wakolosai 2:13-15  Na ninyi mlipokuwa mmekufa kwa sababu ya makosa yenu na kutokutahiriwa kwa mwili wenu, aliwafanya hai pamoja naye, akiisha kutusamehe makosa yote; akiisha kuifuta ile hati iliyoandikwa ya kutushitaki kwa hukumu zake, iliyokuwa na uadui kwetu; akaiondoa isiwepo tena, akaigongomea msalabani; akiisha kuzivua enzi na mamlaka, na kuzifanya kuwa mkogo kwa ujasiri, akizishangilia katika msalaba huo. 

Kilicho muhimu kuliko vyote ni kiki: adui ameshashindwa. Na kama akiweka bunduki kichwani mwako, jua kwamba hamna risasi ndani ya bunduki yake.  Hana uwezo juu ya maisha yako. 

Kama vile Billy Graham alivyosema…  Shetani anapopiga hodi kwangu, mimi huwa ninamwomba Kristo aende kukutana naye mlangoni. 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.