... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Kupanua Upeo wa Macho Yako

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Mathayo 5:7 Heri wenye rehema; maana hao watapata rehema.

Unapomfanya mtu kosa ambalo linaweza kusababisha ubebe matokeo mabaya lakini mtu akaamua kukusitiri, unajisikiaje hapo!?

Ni swali linalovutia, si kweli?  Tunafahamu adhabu tunayostahili, lakini badala yake upande tuliouudhi unaamua kuturehemu. 

Nakumbuku miaka iliyopita pale Wakristo niliyowaudhi kwa makusudi,  watu niliowafanyia yasiyopendeza wakanisaidia na kunipokea nilipofukuzwa kutoka kwenye nyumba yangu niliyopanga. Nakumbuka walivyolia machozi pamoja namimi. Badala ya kunilipa baya kwa baya, wao walinihurumia. 

Ndugu yangu, hii ni rehema.  Na niko hapa pamoja na wewe leo hii kwa sababu wale watu waliamua kunionyesha rehema badala ya kunihukumu kwa haki. Ndio maana Yesu alisema …

Mathayo 5:7  Heri wenye rehema; maana hao watapata rehema. 

Ni rahisi sana kujaribu kuuridhisha ulimwengu unaoendelea kutukumbusha kutetea haki zetu. Ni rahisi kiburi kupanda pale watu wanapotuudhi.  Lakini sasa hivi, mahali tulipo, Yesu anatuita – wewe na mimi – kuwa wenye rehema. 

Ni ajabu kuona jinsi tunavyoweza kutikisa ulimwengu na kuvuta watu kwa Kristo wakati tunaanza kubuni njia za kuonyesha rehema; 

Najua, ni rahisi kunung’unika kwa vile dunia imevyochafuka; kulalamikia maovu yanayotendeka na jinsi watu wanavyotuudhi hata kututesa. 

Lakini mpango wa Mungu ni kutumia watu waliobadilishwa, watu kama wewe na mimi … kubadilisha ulimwengu.  Je! Una fursa gani wewe kuonyesha rehema?  Kwasababu …  heri wenye rehema; maana hao watapata rehema. 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.