... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Sichangamki, Wala Sifurahii, Nipo Nipo Tu

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Ayubu 1:21,22 Akasema, Mimi nilitoka tumboni mwa mama yangu nili uchi, nami nitarudi tena huko uchi vilevile; BWANA alitoa, na BWANA ametwaa; jina la BWANA na libarikiwe. Katika mambo hayo yote Ayubu hakufanya dhambi, wala hakumwazia Mungu kwa upumbavu.

Kuna siku umaamka na huchangamki.  Hata mimi pia huwa ninaamka hivyo.  Tunafahamu kwamba yatupasa kujaa furaha ya Bwana, lakini … hatuchangamki. Sasa itakuaje?

Juzi asubuhi nilikuwa faragha na Bwana – niliomba, Nilisoma neno lake –Si kwamba nilikuwa na tatizo, lakini furaha na amani ninakuwa navyo kama kawaida nikiwa mbele za Bwana.

Kwa hiyo niliomba nikasema, “Bwana, sichangamki, sina furaha, nipo nipo tu.”  Sikuwa na la nyongeza la kusema, ninafikiri Mungu aliridhika.  Yesu alinielewa.  Si alitembea kwa mguu kwenye barabarani zenye vumbi hapa duniani?  Asubuhi ile, Roho aliniongoza nisome mistari ifuatayo: 

Ayubu 1:21,22  Akasema, Mimi nilitoka tumboni mwa mama yangu nili uchi, nami nitarudi tena huko uchi vilevile;  BWANA alitoa, na BWANA ametwaa; jina la BWANA na libarikiwe.  Katika mambo hayo yote Ayubu hakufanya dhambi, wala hakumwazia Mungu kwa upumbavu. 

Kama unafahamu habari za Ayubu, unajua kwamba alipitia majaribu mengi mazito na yenye maumivu. alipokuwa anapitia vipindi vigumu hakuchangamka wala hakufurahi. Lakini imani yake ndani ya Bwana kamwe haikuyumbishwa. 

BWANA alitoa, na BWANA ametwaa. 

Hisia zetu huwa zinapanda na kushuka. Lakini Neno la Bwana linasimama imara pale pale kupitia hali zote. Mungu ni mwaminifu kupitia hali zote na anakupenda kupitia zote.  Ndio maana haijalishi tunajisikiaje, tunaweza kufurahia kupaza sauti na kusema … jina la BWANA na libarikiwe.    

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.