Barua Yako ya Ushuhuda
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
1 Yohana 3:17,18 Lakini mtu akiwa na riziki ya dunia, kisha akamwona ndugu yake ni mhitaji, akamzuilia huruma zake, je! Upendo wa Mungu wakaaje ndani yake huyo? Watoto wadogo, tusipende kwa neno, wala kwa ulimi, bali kwa tendo na kweli.
Swali linalokuja haraka: Je! Wewe ni tajiri kiasi gani? Kwa sababu kama unayo mahitaji ya msingi – maji, chakula, nyumba – basi hata ukijipimaje, wewe ni tajiri kuliko unavyofikiria!
Nilisema jana kwamba nilipata nafasi kutembelea kituo cha wenye ukoma kwenye sehemu ngumu nchini Tanzania. Watu hawa wanakaa kwenye majengo yaliyochakaa ambayo zamani yalikuwa godowni ya bidhaa.
Niliombwa nitoe ujumbe mfupi, baadaye kuwapa kila mmoja mche wa sabuni – kitu cha kawaida lakini muhimu – mikononi mwao, wengi wakiwa na mikono iliyoumbuka hata wegine kukosa vidole kabisa.
Mtu hawezi kutoka sehemu kama hiyo bila kuwa amebadilishwa. Wakati nilifika nyumbani kwetu, mimi na mke wangu tulijaribu kurekebisha utoaji wetu kwa kuzidi kuelekeza msaada wetu kwenye watu maskini. Hakuna jinsi ya kufanya tofauti.
1 Yohana 3:17,18 Lakini mtu akiwa na riziki ya dunia, kisha akamwona ndugu yake ni mhitaji, akamzuilia huruma zake, je! Upendo wa Mungu wakaaje ndani yake huyo? Watoto wadogo, tusipende kwa neno, wala kwa ulimi, bali kwa tendo na kweli.
Kama vile Askofu Mkuu Desmond Tutu aliwahi kusema: “Kila kanisa (na mimi ningeongeza, kila mwamini) lingepaswa kupata barua ya ushuhuda kutoka maskini wanaokaa maeneo yale.”
Ni tamko ambalo linaeleweka kabisa. Kwa sababu shahidi inayokuwa na nguvu kwa kuthibitisha uwepo (au ukosefu) wa wa upendo wa Mungu mioyoni mwetu, ni jinsi tunavyowasaidia maskini.
Na Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.