Bwana Anatupa Matumaini
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
2 Wathesalonike 3:4 Nasi tumemtumaini Bwana kwa mambo yenu, kwamba mnayafanya tulivyowaagiza, tena kwamba mtayafanya.
Unajua ni hisia isiyo ya kawaida kuandaa vipindi hivi vya Neno Safi na Lenye Afya kila siku. Nasema kwa upande wangu; nikiomba, nikiandaa, nikiandika, nikirekodi na kushuti ujumbe mfupi wa Neno la Mungu kwa ajili yako, siku baada ya siku, ni kazi ngumu.
Labda unaangalia Neno Safi na Lenye Afya kwenye TV mara kwa mara, au unasikia kwenye redio au unapokea barua pepe kila asubuhi. Lakini nafikiri hujachunguza namna ujumbe huu umekufikia – na kusema ukweli, siyo lazima ujue.
Kwa sehemu kubwa sijui hata siwezi kuona ni kwa kiasi gani kazi hii ya Mungu imefanya nini moyoni mwako isipokuwa najua machache tu kupitia wale wanaotupigia simu na kutumaujumbe kutujulisha vile Vipindi vya Neno Safi na Lenye Afya vimeleta mabadiliko maishani mwao. hii ni safi kabisa.
kazi yoyote Mungu anayotenda moyoni mwa mtu, ni kazi anayoifanya kupitia Roho wake na Neno lake. Kinachonitia moyo zaidi na kunifanya niendelee kufanya kazi hii ni tumaini langu kwamba Mungu anafanya kazi ndani yako na ndani ya watu wengi wanaopokea ujumbe huu duniani. Na ninamuunga mkono Mtume Paulo pale alipowandikia kanisa la Thesalonike …
2 Wathesalonike 3:4 Nasi tumemtumaini Bwana kwa mambo yenu, kwamba mnayafanya tulivyowaagiza, tena kwamba mtayafanya.
Mimi pia nina matumaini kwasababu ninajua kwamba kuna nguvu ndani ya Neno la Mungu. Kwahiyo, unapolipokea Neno lake moyoni mwako, siku baada ya siku, kumbuka kwamba lengo lake kuu ni kubadilisha kabisa maisha yako; kukuweka huru mbali na mizigo ya dhambi; kukujaza amani na furaha isiyotamkwa.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.